Henry Gemu 20 tu, Ametimuliwa!

Monaco: Henry Ameongoza Gemu 20 tu kisha ametimuliwa!

Klabu ya Monaco imemtimua aliyekuwa meneja wa klabu hiyo ambaye aliwahi kuwa msakata kabumbu maridadi wa enzi zake Thierry Henry. Monaco ambao wanashiriki Ligue 1 wanahangaika kujikwamua kwenye nafasi za hatari mkiani kwenye msimamo wa Ligue 1. Henry ni kama hana bahati hivi na klabu hiyo akiwa ameongoza gemu 20 tu kabla hajatimuliwa!

katika jitihada za kujaribu kuinusuru klabu hiyo isishuke daraja, amefanikiwa kupata ushindi mara tano tu katika gemu za michuano yote. Baada ya kukumbana na rungu hilo, aliyekuwa meneja kabla yake, Leonardo Jardim anatarajiwa kuchukua tena nafasi hiyo.

Hery alitengeneza vichwa vya habari kwenye gemu ya hivi karibuni ambayo Monaco walichapwa bao 5-1 dhidi ya Strasbourg. Baada ya gemu hii Henry alimtukana beki wa wapinzani wake na kisha akaja kuomba msamaha baadae.

Siku kadhaa zilizopita, bwana huyu alinukuliwa akisema kuwa yeye alikuwa hahofii kuhusu hatma yake klabuni hapo na aliamini uongozi wa klabu hiyo wangefanya maamuzi dhidi yake, japokuwa hakubainisha kama maamuzi hayo yangemuathiri vipi yeye. Amekaa klabuni hapo kwa mizei 3 tu.

Henry anadaiwa kuwa huenda wakuu wa klabu hiyo hawakupendezwa na uamuzi wake wa kuwaondoa baadhi ya wachezaji waliokuwa wanacheza katika kikosi cha kwanza bila taarifa kwa wakuu hao. Hata hivyo, kipimo cha kushinda gemu 2 kati ya gemu 12 pia kinaonekana kutouridhisha kabisa uongozi wa klabu hiyo ukitupilia mbali lugha chafu aliyoitumia kwa beki wa timu ya Strasbourg.

2 Komentara

    Ni mapema mno kumtimua azoee

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.