Kiungo wa klabu ya Ac Milan na timu ya Algeria Ismael Bennacer imeelezwa atarejea kwenye kikosi cha klabu hiyo wikiendi hii baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kiungo Bennacer amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu ikiwa takribani miezi saba, Kwani aliumia katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika mwezi wa nne.Klabu ya Ac Milan ilimkosa kiungo huyo wa kimataifa wa Algeria kwa muda mrefu sana katika eneo la katikati ambapo alikua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo.
Kiungo huyo inaelezwa atakua sehemu ya timu hiyo katika mchezo wa wikiendi hii ambapo klabu ya Ac Milan itashuka dimbani dhidi ya Frosinone, Lakini haijeleweka mpaka sasa kama atacheza mchezo huo.Kiungo Ismael Bennacer alisaini mkataba mpya na klabu ya Ac Milan kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu, Hivo kiungo huyo yupo sana ndani ya viunga vya San Siro akiendelea kuwatumikia mabingwa hao wa zamani wa Italia.