Brahim Diaz Kufanyiwa Upasuaji

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Brahim Diaz anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bega kutoka na majeraha aliyoyapata siku kadhaa zilizopita.

Kiungo huyo anaongeza orodha ya wachezaji wa klabu ya Real Madrid waliopata majeraha, Kwnai klabu hiyo imekua ikiandamwa na majeraha sana siku za hivi karibuni.brahim diazKiungo Brahim Diaz ambaye amereja ndani ya klabu hiyo msimu huu akitokea klabu ya Ac Milan ambapo alikua kwa mkopo, Amepata majeraha ambayo yatamfanya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi fulani na kukosekana ndani ya timu hiyo.

Klabu ya Real Madrid imeandamwa na majeraha sana msimu huu kwnai mpaka sasa wachezaji wake kama Vinicius Jr, Tchouameni, Camavinga, Thibaut Courtois, Eder Militao, Arda Guler tayari wameshapata majeraha msimu huu.brahim diazKuongezeka kwa Brahim Diaz ambaye atafanyiwa upasuaji na ni wazi atakua nje ya uwanja kwa muda kidogo, Hali hii inaendelea kuivuruga klabu ya Real Madrid kutokana na majeraha ambayo yamekua yakiwakabili wachezaji wa klabu hiyo.

Acha ujumbe