Nyota wa Napoli Scott McTominay alipata jeraha dogo la kifundo cha mguu wakati Scotland ikishinda 2-1 dhidi ya Poland siku ya jana na atachunguzwa na madaktari wa klabu hiyo leo.

Kiungo wa kati wa Napoli McTominay alilazimika kutoka nje ya uwanja katika ushindi wa 2-1 wa Ligi ya Mataifa ya Scotland dhidi ya Poland jana.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitolewa nje dakika ya 76 kutokana na ‘jeraha dogo’ kama ilivyoandikwa na The Independent.
Toleo la leo lililochapishwa la Gazzetta dello Sport, linaripoti kwamba McTominay atapimwa na madaktari wa klabu atakaporejea Naples leo.


