Inaripotiwa kuwa mchezaji anayelengwa na Manchester United na Chelsea, Victor Osimhen amekataa kuhama katika dirisha lijalo la usajili, ingawa nyota huyo wa Napoli analenga kuingiza fedha kabla ya hapo.

 

Osimhen Amekataa Kuondoka Napoli Huku Utd na Chelsea Zikimhitaji

Osimhen amefunga mabao 18 kusaidia Napoli kujenga faida ya pointi 15 kwenye msimamo wa Serie A huku ni Erling Haaland wa Manchester City pekee mwenye mabao 26 ndiye anayemshinda katika ligi tano bora za Ulaya msimu huu.


Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Nigeria alifunga katika mechi ya saba mfululizo ya ligi katika mchezo ambao Napoli ilipoichapa Sassuolo mabao 3-0 wiki iliyopita, na kiwango chake cha kuvutia kimeripotiwa kuwavutia wawaniaji wa Ligi Kuu ya Uingereza.

United na Chelsea wote wametajwa kumtaka Osimhen, ambaye rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis anasisitiza hauzwi.

Osimhen Amekataa Kuondoka Napoli Huku Utd na Chelsea Zikimhitaji

Huku akitarajiwa kuisaidia Partenopei kutwaa taji la Scudetto kwa mara ya kwanza tangu enzi ya Diego Maradona ndiyo anayoangazia kwa sasa, mshambuliaji huyo ameacha mlango wazi wa kuondoka mwishoni mwa kampeni.

Osimhen ameiambia ESPN; “Unapofanya vizuri sana, vilabu vikuu kote ulimwenguni vinatazama, haswa katika ligi tano bora. Kuweza kuvutia vilabu hivi vya juu kunaonyesha kuwa ninafanya vizuri, na inanipa motisha ya kufanya mengi zaidi kwa ajili yangu na timu yangu.”

Lakini ninaelekeza nguvu zangu kwa Napoli kwa sasa na wao ndio wenye uamuzi wa mwisho. Nataka tu kuisaidia timu yangu kushinda mechi na kushinda mataji. Mwishoni mwa msimu, tutaona kitakachotokea, lakini hilo si juu yangu ni kwa klabu kuamua. Alisema Osimhen.

Osimhen Amekataa Kuondoka Napoli Huku Utd na Chelsea Zikimhitaji

Napoli watasafiri hadi Eintracht Frankfurt kwa mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa siku ya leo, wakiwa wamefunga mabao 20 katika hatua ya makundi wakiwa na mabao 20 ingawa ni moja tu kati ya hizo lilitoka kwa Osimhen.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa