Parades Kutimkia Roma

Kiungo wa klabu ya PSG raia wa kimataifa wa Argentina Leandro Parades anatarajia kutimkia klabu ya As Roma ya nchini Italia chini ya kocha Jose Mourinho.

Kiungo Leandro Parades alikua akiitumikia klabu ya Juventus msimu uliomalizika kwa mkopo wa msimu mzima, Lakini dirisha hili anataka kujiunga na As Roma kwa uhamisho wa kudumu.paradesKiungo huyo wa kimataifa wa Argentina tayari ameshamalizana na As Roma katika maslahi binafsi na mazungumzo baina ya vilabu yamefikia katika hatua nzuri hivo ni wazi kiungo huyo atajiunga na Roma muda wowote kuanzia sasa.

Mchezaji huyo anatajwa kwenda kuziba nafasi ya kiungo Nemanja Matic ambaye ametimkia klabu ya Stade de Rennes ya nchini Ufaransa,Hivo ni wazi Roma lazima wangehitaji mbadala wa Matic ambaye ndio kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina.paradesKiungo Leandro Parades ambaye alikua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Argentina kilichotwaa kombe la dunia nchini Qatar,Kiungo huyo ameieleza kabisa klabu yake ya PSG nia yake ya kutimkia nchini Italia kujiunga na As Roma.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.