Thuram Aweka Kipaumbele Chake Inter Msimu Ujao

Mshambuliaji wa Inter, Marcus Thuram anahisi kuwa anaweza kumaliza msimu akiwa na mabao 20 na asisti 20 siku zijazo akisema kuwa utakuwa ni wakati bora zaidi wa maisha.

Thuram Aweka Kipaumbele Chake Inter Msimu Ujao

Mshambuliaji huyo wa Inter na Ufaransa Thuram anaamini yuko katika wakati mzuri zaidi wa maisha yake ya soka na anafikiri kwamba hivi karibuni anaweza kumaliza msimu mmoja akiwa na mabao 20 na asisti 20.

Mchezaji huyo wa alijiunga na Inter kwa uhamisho bure msimu uliopita wa joto na kushinda taji la Serie A katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo.

“Nilikubaliwa haraka na mashabiki wa Inter, Kusikia jina lako likizungumzwa na mashabiki elfu 75 inasisimua, na unapopenda unachofanya, na una shauku kubwa kama yangu, unaweza kuthamini tu.” Mshambuliaji huyo aliiambia Le Monde.

Thuram amesema kuwa hajiwekei mipaka baada ya msimu kama huu. Yuko katika wakati bora zaidi wa kazi yake na amethibitisha kuwa anaweza kuimarika kila mwaka, kimbinu na kulingana na takwimu.

Thuram Aweka Kipaumbele Chake Inter Msimu Ujao

Chini ya Simone Inzaghi, Thuram amekuwa akicheza kama mshambuliaji wa kati, jukumu ambalo anaweza kulishughulikia akiwa na timu yake ya taifa pia.

“Jukumu la winga ni la zamani, mimi ni mshambuliaji leo,  nataka kuleta mabadiliko katika michezo mikubwa na pia na timu ya taifa.”

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa amethibitisha anaweza kufanya makubw ana anafikiria anaweza kumaliza msimu akiwa na mabao 20 na pasi za mabao 20.

Hapo awali, walinijua kwa sababu nilikuwa mtoto wa Lilian Thuram. Sasa, mimi ni Marcus Thuram, bila kumvua chochote baba yangu ambaye amecheza mechi 142 akiwa na Ufaransa. Ameongeza mchezaji huyo.

Thuram Aweka Kipaumbele Chake Inter Msimu Ujao

Thuram mwenye miaka 26, amefunga mabao 15 na kutoa asisti 14 katika mechi 46 katika mashindano yote msimu huu.

Amejumuishwa kwenye kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya Euro 2024. Alianza kucheza kwa mara ya kwanza akiwa na taifa hilo mnamo Novemba 2020 na amefunga mabao mawili katika mechi 18 akiwa na Les Blues.

Acha ujumbe