Makubaliano baina ya klabu ya Juventus na aliyekua kocha wa klabu ya Bologna raia wa kimataifa wa Italia Thiago Motta yapo sawa mpaka wakati huu.
Juventus ambao wameachana na kocha wake wa muda mrefu Massimiliano Allegri wiki kadhaa zilizopita, Wamekua wakifanya mazungumzo na kocha Thiago Motta kwajili ya kupata saini yake kuelekea msimu ujao wa 2024/25.Taarifa zinaeleza kila kitu kipo sawa mpaka sasa na kocha huyo atasaini mkataba mpaka mwaka 2027 kuwatumikia vibibi vizee hao wa Turin, Huku akiwa na kazi moja tu ambayo ni kurudisha utawala wa klabu hiyo kwenye soka la Italia.
Klabu ya Bologna mpaka sasa inaelezwa kutafuta saini ya kocha mwingine kwajili ya kuziba nafasi ya Motta, Kocha ambaye anafanya mazungumzo na Bologna kwasasa ni Vincenzo Italiano na mpaka sasa wamefikia katika hatua nzuri.Kocha Thiago Motta anaondoka Bologna akiwa amefanya kazi kubwa sana ndani ya klabu hiyo, Kwani amefanikisha kuipeleka klabu hiyo ligi ya mabingwa msimu ujao, Hivo kinachosubiriwa ni kuona kama ataweza kuirudisha klabu ya Juventus kwenye ubora wake.