Yann Sommer Kumrithi Onana

Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kumsajili aliyekua golikipa wa klabu ya Bayern Munich raia wa kimataifa wa Uswisi Yann Sommer kama mrithi wa Andre Onana.

Klabu ya Inter Milan imefikia makubaliano na Bayern Munich ya kumsajili Yann Sommer kwa kiasi cha Euro milioni 6 ambaye ni wazi anakwenda kua golikipa namba moja wa klabu hiyo kuelekea msimu wa mwaka 2023/2024.Yann sommerInterezionale Milan ni wazi ilihitaji golikipa mpya tena mwenye ubora baada ya kumuuza golikipa wake mahiri Andre Onana kwenda klabu ya Manchester United na sasa wamefanikiwa kumpata golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Uswisi.

Golikipa huyo wa zamani wa Borussia Monchengladbach atasafiri siku ya jumapili kuelekea nchini Italia kuhakikisha anakamilisha dili lake la kuhamia klabu ya Inter Milan wanafainali wa ligi ya mabingwa msimu uliomalizika.Yann sommerGolikipa Yann Sommer atafanya vipimo vya afya siku ya jumatatu akiwa tayari ameshafika nchini Italia baada ya hapo atasaini kandarasi ambayo haijawekwa wazi mpaka sasa lakini ni uhakika golikipa huyo atakipiga Inter Milan msimu ujao.

Acha ujumbe