Golikipa kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga Yann Sommer anatajwa kama mbadala wa golikipa namba moja wa klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer.

Golikipa wa klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer ambaye atakosekana msimu mzima uliobakia baada ya kufanyiwa upasuaji, Hivo klabu ya Fc Bayern Munich inatafuta mbadala wa kipa huyo ambaye amepata majeraha.yann sommerGolikipa Yann Sommer raia wa Uswisi amekua kwenye kiwango bora sana kwenye klabu yake ya Borussia Monchengladbach na timu ya taifa ya Uswisi hivo anatizamiwa kua mbadala wa Manuel Neuer ndani Fc Bayern.

Taarifa zinaeleza kua klabu ya Fc Bayern Munich ipo kwenye mazungumzo na golikipa huyo raia wa Uswisi ili kwenda kuzipa nafasi ya Manuel Neur akishirikiana na golikipa chaguo la pili ndani ya klabu hiyo Ulreich.yann sommerYann Sommer amekua akihusishwa na vilabu tofauti kabla ya Bayern Munich, Klabu ya Manchester United nayo ilishaingia kwenye mawindo ya golikipa huyo na hii inakuja kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha golikipa huyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa