Kapu la Fununu za Usajili Ulaya

Ikiwa wiki moja imewasalia kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari, klabu nyingi barani Ulaya zinafanya kila linalowezekana kuweza kuendana na kasi hiyo kwa kusajili wachezaji watakaoziba nafasi zilizokuwepo katika mzunguko wa kwanza wa ligi. Kuna wachezaji ambao walikuwa kwenye malengo ya klabu nyingi ambao inaonekana bado kuna utata kuwanasa.

Barcelona wanawavizia Manchester kumtaka Mata, mabingwa hao wa Hispania wanamhitaji mchezaji huyo na tayari hadi sasa wamekwisha fanya hatua za mwanzo kujaribu kuwasiliana na wakala wake na mchezaji mwenyewe juu ya matamanio yao kutaka kumfanya atue kikosini kwao. Mchezaji huyo amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi ndani ya klabu yake na kwa sasa kandarasi yake imesalia miezi sita tu kuweza kukatika; na yupo huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote ile. Japo wao Manchester bado wanamhitaji mchezaji huyo na kwa mazingira yalivyo hawaonekani kama watamuuza mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wao.

Suarez anataka kutimkia Arsenal, mshambuliaji wa Barcelona, Denis Suarez bado anatamani kutimkia Uingereza kwa sasa na anaona kama hakuna kinachoshindikana kwake kufanya hivyo. Anaamini kwamba Barcelona na Arsenal wanaweza kukaa upya kuyajenga baada ya makubaliano ya awali kuonekana yamefeli kabisa. Wawili hao walishindwa kufikia mwafaka baada ya Barcelona kutaka ndani ya mkataba huo wa Suarez kutua kwa mkopo klabuni hapo kuwepo na kifungu kitakachotaka mchezaji huyo asajiliwe kabisa na klabu hiyo sio kutua kwao kwa mkopo tu. Kutokana na hilo Barcelona wanahusishwa na kumuuza mchezaji huyo kwa Sevilla au Real Betis kitu ambacho Suarez anaonelea ni bora akabadili maamzi ya waajiri wake mapema.

City wanataka kifungua kibubu tena, baada ya kumkosa Frenkie de Jong wanataka kurejea sokoni tena kumnasa mchezaji mwingine ili waweze kukidhi haja ya kikosi chao. Kwa sasa nguvu zote wamezihamishia kwa  Matthijs de Ligt ambaye ameonekana kuwa na uwezo mzuri uwanjani na wanaamini kunufaika sana mchezaji huyo. Kama watakuwa tayari kumsajili mchezaji huyo watalazimika kuwalipa Ajax kitita cha $A92M ili kumsajili kwao. Kutua kwa mchezaji huyo kutapelekea kuondoka kwa beki wa muda mrefu wa kikosi hicho Otamendi ambaye ametumikia kwa muda kikosini hapo. Na huenda naye akaelekea kujiunga na Barcelona.

James sio wa Arsenal, washika bunduki sasa wanaonekana kukosa kila chaguo wanalolihitaji; hii ni baada ya Rodriguez ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo na Bayern kutaka kurejea kwenye klabu yake ya awali na kitojiunga na upande wowote mwingine. Mchezaji huyo yupo tayari kurejea kupigania namba yake ya kudumu ndani ya kikosi cha matajiri hao zaidi ya kwenda kujinga na Arsenal. Japo maisha yake kwa sasa ana furaha sana kuwepo chini ya Bayern na anaamini ni klabu kubwa sana kwake. Ndani ya moyo wake anamapenzi makubwa na Madrid na furaha yake kubwa ni kuendelea kuwa na Madrid siku zote, na yupo tayari kurejea kikosini hapo muda wowote. Kwa kiwango anachokionesha sasa hivi mchezaji huyo hakuna ugumu wowote utakaojitokeza juu ya yeye kurejea kikosini hapo.

3 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.