Nyota wa PSG, Neymar alisepa dimbani akitoa machozi kwenye gemu waliyopata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Strasbourg ya kombe la Ufaransa. Alitoka kwa sabu baada ya kupata jeraha, huenda ndio kilichomliza kwa sababu ya maumivu makali.
Kabla hajapata jeraha, Neymar alichezewa rafu mara 3 na mpinzani wake Moataz Zemtemi, akaamua kumfanyia vimbwanga vya kumpitishia mpira juu yake kama kanzu vile!
Nyota huyu wa miaka 26 anafahamika kwa staili yake ya mpira wa maringo na kupenda kuhangaisha wapinzani kwa chenga za hapa na pale nyingi zikiwa ni zile za kuwaacha watu midomo wazi.
Lakini kwenye gemu hii nyota huyu alijikuta akitoka uwanjani anamwaga machozi baada ya kupata jeraha kwenye kiungio cha mguu wake wa kulia karibu na kisigino, alipata jeraha hili baada ya kuukanyagia mguu vibaya wakati akikimbia. Neymar alishawahi kupata jeraha kama hili na kulazimika kukosa gemu 17 za timu yake.
Ni kama alipaniwa na wapinzani wake ambao wanalaumu aina ya uchezaji wake. Jeraha la Neymar limekuja wakati mgumu kwa klabu ya PSG wakiwa bado wana vibarua vigumu mbele yao ikiwepo pamoja na gemu dhidi ya Manchester United.
Mmoja wa wapinzani, Anthony Goncalves amenukuliwa akisema “ni mchezaji mkubwa sawa. Lakini staili yake ya kucheza, ukicheza kama hivi basi usije ukalaumu ukichezewa rafu.”.
Taarifa za kitabibu bado hazitatoka kuelezea kwa kina kama ni mda gani haswa nyota huyu atasalia nje ya dimba akiuguza jeraha lake. Hata hivyo vtaarifa ya klabu hiyo inasema madaktari wanasema uwezekano wake wa kutibika mapema utategemea uwezo wake wa kurejea hali nzuri siku hizi chache.


Povel
Gud news