Mchezaji Philippe Coutinho hali yake katika klabu ya Barcelona ipo katika hali ambayo haieleweki. Hii ni baada ya maisha yake ya kisoka ndani ya klabu hiyo kwenda nje ya kile alichokuwa akikifikiria kwa kipindi kirefu kwamba angejenga historia kwa kujiunga na klabu hiyo yenye historia kubwa katika soka.
Coutinho alijiunga na Barcelona Januari, 2018 akitokea Liverpool kwa uhamisho uliokuwa wa kihistoria ndani ya klabu hiyo. Aliondoka klabuni hapo akiwa na historia kubwa na rekodi ya aina yake ndani yake, lakini mambo yanaonekana tofauti kwa sasa; katika klabu yake hiyo mpya anayohudumu kwa sasa. Amekuwa ni mchezaji anayesugua benchi na kupata nafasi chache sana za kuonesha ubora wake uwanjani.
Maisha yake yanaendelea kukaa upande mbaya kutokana na ripoti zinazoendelea kwamba klabu hiyo ipo mbioni kumrejesha Mbrazil mwenzake Neymar kutoka PSG kitu ambacho kitamkosesha namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho. Kutokana na nafasi za wachezaji hao uwanjani.
Haya yote yakiwa yanatokea, kocha wake wa zamani aliwahi kumtahadharisha mchezaji juu ya tabia ya klabu hizo kubwa na tabia wanazowafanyia wachezaji wa aina yake. Kitu ambacho Coutinho hakuweza kukisikiliza kabisa na kuondoka klabuni hapo. Kitu ambacho hadi sasa kitakuwa kinamuumiza mchezaji huyo kutokana na kupuuza maneno aliyopewa na mwalimu wake hapo awali.
Baadhi ya vitu alivyowahi kumwambia mchezaji huyo ni kwamba, ni bora asalie klabuni hapo kwa sababu itamsaidia yeye kujenga jina lake na heshima ya timu anayochezea; kwenda katika klabu zenye majina kama Barcelona na Madrid kungemfanya mchezaji ndio lakini mwenye kuwajenga wachezaji wengine. Akiwa na maana atafanya kazi katika vivuli vya wachezaji wengine na thamani yake haiwezi kuonekana waziwazi. Maneno haya yanadhihirika sasa kutokana na hali anayopitia mchezaji huyo kwa sasa.
Msimu huu mchezaji huyo amefanikiwa kuanza mechi tisa tu akiifungia timu hiyo magoli manne na kutoa pasi ya goli moja: huku akiwa ameingia akitokea benchi mara saba. Takwimu hizi ni tofauti kabisa na zile alizowahi kuzipitia akiwa na klabu nyingine. Amekuwa zaidi mbadala badala ya kuwa mchezaji tegemezi katika timu. Hili ni suala ambalo mchezaji wa aina yake linaweza likachangia kushusha uwezo wake.
Pamoja na kutompa nafasi kubwa ya kuonesha makali yake, lakini klabu hiyo bado ipo bora hoyo ni dalili kwamba hawategemei sana huduma yake ndani ya kikosi hicho. Mbali na mchezaji huyo pia mchezaji mwenzake Ousmane Dembele naye yupo katika kipindi kigumu cha kuweza kudhihirisha ubora wake ili aweze kuaminiwa kikosini hapo.
Povel
Duh