Kombe la Dunia 2026 Hatihati Kuchezeka Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameibua taharuki kubwa kuhusu maandalizi ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, akitoa kauli kali kwamba yuko tayari kuhamisha mechi kutoka miji iliyopangwa endapo ataona kuna hatari ya kiusalama. Kauli hiyo imeweka shinikizo kwa Rais wa FIFA Gianni Infantino, ambaye uhusiano wake wa karibu na Trump sasa unazua maswali kuhusu uhuru wa taasisi hiyo ya kimataifa.

Kombe la Dunia 2026 Hatihati Kuchezeka Marekani

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, Trump alisema: “Kama nitaona mji si salama, tutahamisha mechi. Bila shaka tutaliamisha Kombe la Dunia. Hatutaruhusu kufanyika katika mji wowote wenye hatari hata kidogo.”

Kauli hiyo imeibua hofu kwamba uingiliaji wa kisiasa unaweza kuvuruga mchakato wa FIFA wa kuchagua miji mwenyeji, mchakato unaojumuisha zabuni, mikataba, ziara za tathmini, na makubaliano ya kimasoko na miundombinu.

Ingawa Chicago haimo kwenye orodha ya miji mwenyeji, Trump alitaja takwimu za uhalifu katika jiji hilo kama mfano wa miji isiyo salama. Hii imefanya wachambuzi waone kuwa miji inayojulikana kama ‘sanctuary cities’ ambapo ushirikiano na maafisa wa uhamiaji wa ICE umepunguzwa inaweza kuwa kwenye hatari ya kuondolewa kwenye ratiba.

Kombe la Dunia 2026 Hatihati Kuchezeka Marekani

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Miji kama New York, Boston, Seattle, San Francisco na Los Angeles iko kwenye orodha ya miji yenye msimamo mkali dhidi ya sera za uhamiaji za Trump, na tayari imetishiwa kukatwa ufadhili wa serikali kuu.

Kufuta mji mmoja au zaidi si suala la kubadilisha ratiba tu. Athari zake ni kubwa ikiwemo kambi za mazoezi za timu, ratiba za safari za mashabiki na timu, makubaliano ya kibiashara na wadhamini pamoja na usalama wa miundombinu ya michezo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.