Savinho Asaini Mkataba Mpya City, Tottenham Wapigwa Chenga

Ndoto za Tottenham Hotspur kumsajili winga wa Kibrazil Savinho zimeyeyuka rasmi baada ya Manchester City kuthibitisha kumfungia mkataba mpya hadi mwaka 2031. Kwa mujibu wa The Athletic, City wamechukua hatua ya haraka kuzuia majaribio ya Spurs ya kumvuta nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye walikuwa wakimnyemelea tangu dirisha la kiangazi.

Spurs walikuwa na matumaini makubwa ya kumshawishi Savinho kujiunga na mradi wa Thomas Frank, wakimwona kama suluhisho la haraka kwa safu yao ya ushambuliaji. Lakini City walifunga milango yote ya mazungumzo, wakisisitiza kuwa mchezaji huyo si wa kuuzwa.

Savinho Asaini Mkataba Mpya City, Tottenham Wapigwa Chenga

Baada ya kukosa mechi tatu za mwanzo wa msimu kutokana na majeraha, Savinho amerudi kwa kishindo. Alifunga bao lake la kwanza msimu huu katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Huddersfield kwenye Kombe la Carabao, akimkumbusha Pep Guardiola kwa nini aliamua kumbakiza Etihad.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Katika msimu wake wa kwanza na City, Savinho alicheza mechi 48, akifunga mabao matatu na kutoa pasi za mabao 13 takwimu zinazomfanya kuwa mmoja wa wachezaji chipukizi wenye mchango mkubwa barani Ulaya.

Savinho Asaini Mkataba Mpya City, Tottenham Wapigwa Chenga

Kocha mkuu Pep Guardiola hajawahi kuficha mapenzi yake kwa Savinho. Tangu mwezi Agosti, alieleza wazi kuwa winga huyo ni sehemu ya mipango yake ya muda mrefu, akipuuza kabisa tetesi za usajili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.