Kiungo mkongwe wa zamani wa FC Barcelona na sasa nyota wa Inter Miami, Sergio Busquets, ametangaza rasmi kuwa atastaafu soka mwishoni mwa msimu huu wa Major League Soccer (MLS), akimaliza safari ya kipekee ya karibu miaka 20 uwanjani.
Busquets, mwenye umri wa miaka 37, alithibitisha uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akisema: “Nahisi muda umefika wa kusema kwaheri kwa taaluma yangu ya uchezaji soka. Imekuwa takriban miaka 20 ya kuishi ndoto yangu ya utotoni.”
Busquets anaacha alama isiyofutika katika historia ya soka duniani akifanikiwa kuchukua Kombe la Dunia (2010) akiwa na Hispania, Ubingwa wa Ulaya (Euro 2012), Ubingwa wa La Liga mara 9, Kombe la UEFA Champions League mara 3, Copa del Rey mara 7, na mechi 137 za kimataifa akiwa na La Roja.
Alianza safari yake kupitia kituo cha mafunzo cha La Masia, akapanda hadi kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka 2008 chini ya Pep Guardiola, ambapo aligeuka kuwa injini ya mfumo wa tiki-taka uliotawala Ulaya kwa miaka mingi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Mnamo 2023, Busquets alijiunga na Inter Miami ya Marekani, akicheza sambamba na wachezaji wenzake wa zamani Lionel Messi, Jordi Alba na Luis Suárez. Ujio wao uliibadilisha Miami kuwa timu ya ushindani, na sasa wamefuzu kwa hatua ya mtoano (playoffs) ya MLS.



