Baada ya mizunguko mingine kukamilika na washindi kupatikana; klabu nyingi zitakuwa zinaelekea kutafuta nafasi ya kusonga mbele katika mzunguko unaofuata. Katika mechi hizo itashuhudiwa timu kubwa zikimegana na timu kubwa zikikanyagana zenyewe ili kupata washindi. Klabu kama Chelsea na Man City zinapewa nafasi ya kusonga kutokana na uwezo wa wapinzani wao kuwa chini “Underdog”. Lakini, katika soka kuna maajabu lolote linaweza kutokea na likamkuta yeyoye.
Liverpool akiwa ametupwa nje ya michuano hiyo kwa kupokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Wolverhampton. Haikuwa rahisi kuona klabu kubwa kama hiyo ikipokea kichapo hicho na kupotezwa kabisa mchezoni kitu ambacho katika soka kinawezekana. Kwa uwezo wa klabu hiyo kwa wakati uliopo ilitazamiwa angeweza kupata nafasi ya kusonga mbele zaidi.
Kuelekea hatua ya 32 bora za michuano hiyo, Arsenal atakuwa mwenyeji wa Manchester United katika hatua inayofuata huku zikiwa ni timu pekee kubwa zinazokutana katika hatua hiyo. Katika mchezo huo itashuhudiwa soka safi ambalo litachezwa chini ya uongozi mpya baada ya mechi iliyopita, zilipokutana timu hizi kutopatikana mbabe. Lakini awamu hii lazima mbabe apatikane ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo yenye heshima kubwa.
Mabingwa wa ligi kwa msimu uliopita, Man City wao watakuwa na kazi nyepesi kuweza kuwararua Burnley ambao hawajawa na matokeo mazuri hata katika ligi ya ndani. Ba faida aliyopewa Man City ni kwamba ataicheza mechi hii mbele ya mashabiki wake wote katika uwanja wa nyumbani. Kwa faida hiyo sio rahis kusema Burnley ataweza kupindua meza na kumfunga City kwenye viunga vyake.
Chelsea wao watakuwa na kazi nyepesi pia kuweza kumaliza biashara na Sheffield Wednesday or Luton. Ikumbukwe kwamba wao ndio wanaoshikilia kombe hilo kwa sasa, hivyo wapo katika hatua nzuri ya kusonga mbele japo safu yao ya ushambuliaji imekuwa butu sana kiasi cha kushindwa kufunga magoli mengi suala ambalo lina athari sana kwenye michuano hii.
Tottenham watakuwa na kibarua kizito mbele ya Crystal Palace baada ya wao kupata ushindi mnene wa magoli 7-0 mwishoni mwa wiki. Crystal palace sio timu ya kubezwa wanapokutana na kigogo; hufanya kila wanaloweza kuzuia wasipoteze ushindi wao kirahisi. Tena Tottenham katika mechi hiyo atakuwa ugenini hivyo lolote linaweza kutokea japo anapigiwa upatu wa kusonga mbele zaidi katika mechi hiyo kutokana na nidhamu ya kikosi alicho nacho.
Mechi nyingine zinazoendana na hizo, ambazo zitapigwa ndani ya Januari 25 na 28 ni Swansea v Gillingham, Shrewsbury or Stoke v Wolves, Millwall v Everton, Bristol City v Bolton, Accrington v Derby or Southampton, Doncaster v Oldham, Newcastle or Blackburn v Watford, Middlesbrough v Newport, Barnet v Brentford na Portsmouth dhidi ya QPR.


Furahav
Iko poa.
Povel
Habar njema