Mlinda lango wa klabu ya Liverpool, Loris Karius amevunja mkataba wake wa mkopo na Klabu ya Besiktas ya Uturuki, na mlinda lango huyo akitoa sababu kuwa ni kutolipwa mshahara tangu Januari… Karius amekuwa kwa mkopo huko Besiktas tangu 2018 na alikuwa anatakiwa kurejea katika Klabu yake ya Liverpool mwishoni mwa msimu.

Mjerumani huyo alienda kuwashitaki Besiktas mwezi uliopita alipogonga mlango huko Shirikisho la Soka Duniani “FIFA” na kuomba ruhusa ya kuvunja mkataba wake na Klabu hiyo. Kipa huyo anadai kuwa hajapata kupokea mshahara wake kutoka kwa Besiktas tangu Januari na sasa amechukua hatua ya mwisho kukomesha mkataba wake na The Black Eagles.
Hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Klabu, lakini kwa upande wake Karius Amethibitisha kuwa yeye sio mchezaji tena wa Besiktas…Anatarajiwa sasa kurudi Liverpool, ambapo bado yuko chini ya kandarasi nao, Liverpool ambao wamehusishwa na kutaka kumuuza msimu huu wa joto na klabu ya kwao Ujerumani, Werder Bremen ikimuhitaji..


mathayo sonje
nilijua ni bongo ndo wachezaji wanachelewa kulipwa mishahara kumbe hadi majuu pia, hii ndio faida ya kujiunga na meridianbet maana wanatupa habari motomoto
Ernest Kimeru
Watu tunajuwa haya Mambo Ni Bongo tuu kumbe adi ulaya???!!!!!
Hamidu
Moja wa golikipa mbovu wa liverpool. ..namkumbuka mechi ya fainal ya real madrid alichomesha.
Frank patrick
Dah bora apate team ya kucheza huyu jamaa na afute makosa yake…YNWA
Lombo
duuh kumbe janja janja sio bongo tu
Povel
Harud nyumban aje kujipang upya kuanza moja so ujinga
Ester mmakasa
Jamani mpaka nje wanakuwa wababaifu kwa wafanyakazi wao.
Rehema Dickson
Me nikaju kwetu tu kumbe adi uko mambo aya yapo du
Adelta
Nilijuwa hapa kwetu tu ndiy kunashida ya
Mshahar kumbe hata kwa wenzetu
Kwel Hali Ni ngum
Mariam
Bora arudi
Genia Sikaluzwe
Tunajuwa ni hapa bongo tu kumbe hata kwa wenzetu haya Mambo yapo duuuuh hatari