Jurgen Klopp: Ninajisikia Raha Sana kwa Liverpool

Jurgen Klopp anasema ana furaha sana kutokana na ubora wa kikosi chake kwa sasa. Bosi huyo wa Liverpool inayokipiga kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, Jurgen Klopp amesema kwamba bado anafurahishwa sana na kikosi chake cha kwanza cha klabu hiyo.

Katika madirisha matatu ya usajili ambayo yamepita klabu imetumia fedha kidogo sana katika usajili wa wachezaji wapya. Kwa sasa ni wazi kabisa kwamba Liverpool ndiyo klabu ambayo inapigiwa upatu kuja kuwa na utajiri mkubwa wa wachezaji.

Hata hivyo, ingawa wanaunganishwa kwenye dili za watu kama akina Jadon Sancho na Timo Werner, Klopp amesisitiza kuwa ametosheka sana na wachezaji ambao anao kwa sasa katika mikono yake klabuni pale.

Akiongea na beIN Sports, Mjerumani huyo anasema kuwa: “Sadio Mane ni kijana anyetosha kabisa na Mo Salah bado ni kijana muhimu kwetu na watakuwa hivyo kwa miaka kadhaa ijayo. Nina furaha sana kwa kweli, siwafikirii kabisa wengineo walio nje ya klabu.

Jurgen Klopp anasema ana furaha sana kutokana na ubora wa kikosi chake kwa sasa. Bosi huyo wa Liverpool inayokipiga kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, Jurgen Klopp amesema kwamba bado anafurahishwa sana na kikosi chake cha kwanza cha klabu hiyo.

“Nikiwa mazoezini na vijana wangu huwa sifikirii kabisa juu ya usajili wa wachezaji wengine. Kama tutasajili mbeleni tutaangalia uwezekano lakini kwa sasa tutatumia hawa hawa tulionao kikosini.”

Kwa sasa klabu yake ya soka ya Liverpool ina alama 25 zaidi ya yule anayefuatia kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Premier League.

17 Komentara

    Liverpool ni klabu bora kwa msimu huu na msimu ujao kama wachezaji maarufu wasipoondoka kama Sadio Mane,Firmino,Robertson,Van Dijik na Trent Arnold

    Jibu

    sehemu unapopata mafanikio lazima ufurahie kama Klopp anavvofurahia kuwa Liverpool, maana ni timu yenye mafanikio makubwa kwa msimu huu.

    Jibu

    Klop ni kocha Bora Sana na kaweza kuendana na falsafa ya Liverpool ni jambo la furaha kwake

    Jibu

    Inafanya vizuri Liverpool hata mm nafurahia ilinapcheza.

    Jibu

    Liverpool inafanya vzr sana napia huyo kocha jurgen klopp na namkubali sana

    Jibu

    Inafanya vizuri Liverpool hata mm naifurahia inapocheza uwanjani.

    Jibu

    Klopp anastahili heshima kwa Mambo makubwa aliyoifanyia Liverpool kwa wakati huu.

    Jibu

    Liverpool ni club Bora,huwa inajua nini inafanya poa hawajakosea hata lile neno la kwenye nembo yao,,,,I will never walk alone,safi sana kwa Liverpool chama la wana

    Jibu

    anahitajika kusajili hata wawili or amrudishe wilson na grujic aache kujiamini sanaa….YNWA

    Jibu

    liver wamekamilika haina haja ya usajili

    Jibu

    Liverpool Ni klabu nzuri Sana
    Hawaitaji usajili

    Jibu

    Jurgen klopp ni bonge la kocha

    Jibu

    Bonge la kocha kwa hv Sasa katika ulimwengu wa soka

    Jibu

    Kocha mzur sana huyu

    Jibu

    Klopp amejitoa Sana kuhakikisha Liverpool imefika mbali

    Jibu

    Ameisaidia sana Liverpool kufurahi ni haki yake

    Jibu

    Yuko vizuri sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.