Unadhani ni Di Canio? Zola? Ravanelli? Waliowika walipoichezea ligi kuu ya Uingereza?
Ni moja ya taifa ambalo limekuwa na vipaji lukuki na wachezaji bora sana waliotisha walipokuwa ama wawapo ndani ya ligi kuu ya EPL nchini Uingereza.
Wamekuwa na staili za aina yake na manjonjo makubwa sana wawapo uwanjani, hawa jamaa wameshinda FIFA World Cup mara nne na wameenda wakafanya vyema kule Uingereza.
Tangu kuanza kwa msimu wa soka wa mwaka 1992/93 kumekuwa na jumla ya wachezaji 76 waliowakilisha taifa la Italia kwenye Premier League, akiwemo Andrea Silenzi ambaye amekuwa ni wa kwanza alipoichezea klabu ya soka ya Nottingham Forest mwezi Agosti mwaka 1995.
Mojawapo ya mabao yaliyoweka historia ni yale ya akina Di Canio, Carbone, Zola, Pelle na wengineo wengi sana kutokea Italia.
Ubora wa Gianfranco Zola alipokuwa kwa klabu ya Chelsea alikuwa ni mchezaji muhimu sana kwa kufunga jumla ya magoli 59 na kusaidia upatikanaji wa mengine 42 kwa klabu hiyo.
Alikuwa na wenzake kutoka huko akiwemo Roberto Di Matteo pamoja na Gianluca Vialli, ambao wote hawa waliiwezesha klabu ya The Blues kushinda mataji kadha wa kadha huko Ulaya.
Ni Paolo Di Canio pekee ambaye amemzidi Zola ukiangalia kwa wale waliotokea Italia. Amefunga jumla ya mabao 66 na kusaidia mengine 49 akiwa na klabu za soka za Sheffield Wednesday, West Ham United na baadaye Charlton Athletic.
Takwimu zinazoongoza kutokea kwa wachezaji wa Italia waliocheza ndani ya PL
| Mechi | Magoli | Assists | |||
|---|---|---|---|---|---|
| Gianfranco Zola | 229 | Paolo Di Canio | 66 | Paolo Di Canio | 49 |
| Paolo Di Canio | 190 | Gianfranco Zola | 59 | Gianfranco Zola | 42 |
| Benito Carbone | 177 | Benito Carbone | 35 | Benito Carbone | 35 |
| Carlo Cudicini | 161 | Fabrizio Ravanelli | 25 | Roberto Di Matteo | 13 |
| Alessandro Pistone | 149 | Graziano Pelle | 23 | Gianluca Vialli | 11 |
Fabrizio Ravanelli aliwika ghafla akiwa katika klabu ya Middlesbrough msimu wa 1996/97, alifunga hatitriki katika wikiendi ya ufunguzi wa msimu akiwa na klabu yake dhidi ya Liverpool na kufunga jumla ya mabao 16, akawa sawa na Di Canio katika ubora kwenye msimu mmoja.
Kwa upande mwingine Benito Carbone alizichezea klabu tano tofauti ndani ya Premier League akiwa na klabu ya Sheffield Wednesday ambako alifanya vyema zaidi ya kokote alikokuwa.
Angalia takwimu bomba zaidi hapo juu kwenye jedwali na utuambie unadhani ni nani alifanya vyema akiwa Premier League alipotokea Italia?
- Benito Carbone
- Paolo Di Canio
- Roberto Di Matteo
- Fabrizio Ravanelli
- Gianluca Vialli
- Gianfranco Zola


Sylvester
Zola alikua bora sana kati ya hao kwa upande wangu.
Ernest Kimeru
Di Canio hatari hapa ukiangalia records.
Adelta
Mim namkubali Sana zola
Lombo
meridianbet hamjawai mpo juu kwa habar moto moto
Frank patrick
Me nilikuwa namkubali sana Zola namba ya jersey yake ikastaafishwa kabisa pale chelsea
Njiku
Paolo di canio yupo poa
Povel
Nilikuwah cjui Kama wababe wote wamekipgah sana nakukichafua vibaya sana Asante kwa habar Moto moto
Hopemwaikux
Axante kwa habar zenu nzur nzur
Ester mmakasa
Na ndo maana inaonekana kama ligi bora duniani kwa kuwa na wachezaji bora kutoka pande zote duniani.hao jamaa walikua ni hatari sana
Gabriel
Good news 👍
aisha
Habari njema
christopher
Graziano Pelle , hajafanya maajabu makubwa sana ila napenda style yake ya uchezaji alikvyokuwa pale southampton
Rehema Dickson
inaonekana kama ligi bora duniani kwa kuwa na wachezaji bora kutoka pande zote duniani.hao jamaa walikua ni hatari sana