Straika wa Juventus Mario Mandzukic amechomoa ofa ya kuhama Juventus na kujiunga na mashetani wekundu. Mwanzo ililipotiwa kuwa Mourinho alikuwa anamfukuzia straika huyo kwa mbinde. Mario Mandzukic ambaye ana umri wa miaka 32 aliyetokea Atletico Madrid anakadiriwa kulipwa mshahara wa Euro milioni 3.5, Ofa yake inadaiwa ingeongeza mshahara wake hadi kufikia Euro milion 5 kwa msimu. Mandzukic amecheza mechi 129 toka alivyosainiwa kutoka Atletico madrid amefunga magoli 34.
Mandzukic anadaiwa kuwa ni kweli angeondoka Juventus kwa kuwa Mourinho alijitahidi kufanya juu chini kumpata mchezaji huyo lakini dili haijaenda vyema baada ya Mario Mandzukic kuchagua kubakia Juventus. Meneja wa Juve, Massimiliano Allegri amemuhakikishia Mandzukic kuwa yeye ni mtu muhimu katika kikosi chake, na yeye kwa sasa anafikiria kupata ubingwa akiwa na klabu hiyo.


Povel
Manduzkic mwamba