Lionel Messi anatamani Barcelona imuuze Ousmane Dembele kuliko Philippe Coutinho. Mbrazili huyo kwasasa anahusishwa sana kuondoka Barcelona kipindi hiki cha kiangazi huku Chelsea, Manchester United, Tottenham, Arsenal na Paris Saint-Germain zikiripotiwa kuwania saini yake.
Countinho ametumika msimu mzima akiwa kwa mkopo Bayern Munich mabingwa wa Bundesliga na hawako tayari kukamilisha dili la kumchukua jumla kwa £105m.

Barcelona imebadilisha wazo la kumuuza Countinho mwishoni mwa msimu na ripoti zimesema Messi amekasirishwa na jinsi klabu inavyomchukulia kiungo huyo wa zamani wa Liverpool.
Ripoti zinasema Messi na wachezaji wengine wakubwa wanatamani Dembele auzwe. Ousmane Dembele ana hangaika na majeraha tangu ajiunge na Barcelona 2017. Mchezaji huyo wakimataifa wa Ufaransa alisaini kwa £97m na nyongeza £38m Agosti 2017, anahangaika na majeraha tangu atue Camp Nou ameanza mechi 35 katika misimu mitatu.seasons.


aisha
Mko vizuri sana meridianbet
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa