Messi Anataka Kubamba Zaidi ya CR7

Hawa jamaa ni wapinzani wa Jadi sasa! Christiano Ronaldo -CR7 na Lionel Messi kwa kipindi kirefu wamekuwa wapizani katika ligi ya La Liga, Messi akiwa barcelona wakati Ronaldo akiwa Real Madrid. Ushindani wao umekuwa ukiwavutia wapenzi wa soka kwa mda mrefu zaidi, wamekuwa na jitihada zinazofanana kwa kiasi katika michango yao kwa timu na mafanikio ya vikombe vikubwa.

Messi Anataka Kubamba Zaidi ya CR7

Miezi kadhaa iliyopita Lionel Messi alisikika akidai kuwa amekumbuka uishindani wake na Ronaldo, akisema ulikuwa ni ushindani mzuri kuwahi kutokea. Ronaldo naye katika tambo zake akasema kama Messia anataka ushindani basi amfuate Serie A.

Jamaa hawa wote wanakimbiza wakiwa wametwaa Ballon d’Or 5 huku wakiendelea kukimbizana kwenye rekodi mbali mbali.

Je Ushindani wao unawapa hamasa?

Kuna wadau wanasema kuwa kufanya vizuri kwa jamaa hawa ni kwa sababu ya kutegemeana, yaani uwepo wao wote kwenye gemu. Maneno rahisi wengine wanasema kuwa chochote ambacho Ronaldo anakifanya, Messi atataka kumuonesha kuwa yeye anaweza kufanya kwa bora zaidi.

Acha stori za nyuma, Angalia ligi ya mabingwa msimu huu!

Ronaldo amekuwa sehemu muhimu mno ya klabu ya Juventus, ambao wamekuwa hawana bahati sana ya kuchomoka kwenye mzunguko wa mtoano wa timu 16 na kupenya robo fainali. Mchango wa Ronaldo umeonekana kwa kiasi kikubwa kuivusha timu hiyo kuingia hatua inayofuata hasa kwa Hat-Trick aliyoichapa kwenye gemu dhidi ya Atletico Madrid.

Messi hayupo nyuma hapa, na yeye kwa upande wake amekuwa sehemu muhimu ya Barcelona. Kutokuwepo kwa Messi huonesha pengo kubwa klabuni hapo, takwimu za kwenye Ligi ya Mabingwa zinaonesha namna anavyojaribu kumuonesha Ronaldo kuwa anaweza kufanya zaidi yake.

Messi Anataka Kubamba Zaidi ya CR7
Rekodi ya Messi na Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Je ingekuwaje kungekuwa na Messi bila Ronaldo, au Ronaldo bila Messi?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.