Michael Essien na Mwisho Mbaya wa Historia Yake ya Soka

Bado naikumbuka nusu fainali ya pili ya UEFA Champions league kati ya Chelsea na Barcelona pale Stanford Bridge mwaka 2009. Namkumbuka Michael Essien akipatrol kwenye lile dimba, sijalisahau goli lake mpaka leo. Lile fataki, bado sijalisahau. Bahati mbaya referee Tom Ovrebo alikuwa na siku mbaya kazini, maamuzi yake mabovu yakaiondoa Chelsea, kazi ya Essien usiku ule ikasahaulika, yule mrusi alilihujumu jasho la mwanaume yule.

Bado nalikumbuka goli lake la kusawazisha mbele ya Arsenal ule msimu wa 2006-07. Wale wazungu wangeiambia nini dunia kama wasingelichagua kuwa bao bora la msimu. Bado nalikumbuka lile alilowafunga Valencia, lile lililowapeleka Chelsea nusu fainali ya UEFA mwaka 2008.

Licha ya utashi wake na upendeleo wa kucheza kwenye kiungo wa kukaba, si mtu amabye angelalamika kwenye majukumu mapya. He was a utility player. Umpange full back, beki wa kati au kiungo wa juu. Hii ndiyo sababu iliyomshawishi Mourinho alipe Euro 24 Millioni kumng’oa pale Lyon.

Mapafu yake ya farasi, nguvu zake za Faru na miguu yake ya chuma iliwaaminisha Lyon huyu ni Box to box midfielder na siyo beki wa kati kama walivomuona Liberty professionals. Club yake ya utotoni kutoka kwenye ardhi ya amani ya mzee Kwame Nkurumah nyumbani kwao Ghana.

Pale Chelsea Akicheza katikati ya Makelele na Frank lampard, angekupa kila unachohitaji kutoka kwa kiungo. Ungetaka soka la kitemi angekupa falsafa za Benito Mussolin, ungetaka mpira tulivu angekuonesha moyo wa Alfred Noble, ungehitaji mpira wa ladha angekupa mashairi ya Edgar Allen Poe.
Bado nawawaza waingereza waliomuita “the bisson” bado nawawaza wafaransa waliomuita “the physical monster “. Walishindwa kumpa heshima nyingine kubwa zaidi ya haya majina. Hata bango lenye picha yake pale Stamford bridge kama Torres? Hata jina lake jukwaani pale Parc Olympique Lyonnais?

Bado naulilia ule mpira wa juu alioenda kuucheza ile mechi na Libya. Laiti kama angejua unakuja kuathiri career yake kiasi kile asingethubutu kunyanyua miguu yake kuruka. Alipotua alipata injury ya kifundo cha mguu iliyoufikisha mpira wake mwisho. Daah mwisho mbaya sana.

6 Komentara

    Mourinho alimtumia sana huyu mpaka utamu ukaisha

    Jibu

    Yuko vzur

    Jibu

    Amefanya mambo mengi sana kiwanjani, Kumbukumbu zako bado zitaendelea kuwepo kwenye fikra zetu japo kwasasa ukipigi tena.

    Jibu

    Hakika kweli ni story mana hata mm nikiisoma inavutia kwa kiwango chake katika timu ya Chelsea

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Easein ameacha historia ila majeraha yamemfanya astaafu mapema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.