Msakata kabumbu mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona ambaye ana umri wa miaka 31 raia wa Argentina, Lionel Messi amesema kwamba yeye alishangazwa sana na maamuzi ya mshambuliaji mwenye umri wa miaka 33 wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo!
Ronaldo alisepa Real Madrid kwenda Juventus ya Italia ambapo kwa mujibu wa jarida la AS, Messi ameeleza kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa staa huyo ambaye alikuwa tegemeo kubwa ndani ya kikosi cha Madrid huko Hispania.
Imani ya Messi
Lionel Messi anaamini kuwa ikiwa Ronaldo angesalia klabuni Real Madrid angeweza kuleta ushindani mkubwa sana katika ligi ya La Liga na baina ya timu hizo mbili hasa katika gemu za El Clasico iliyo na ukubwa wa aina yake barani Ulaya.
Kwa sasa Ronaldo tayari ameshajiunga na klabu ya Juventus ya Italia na tayari ameshakipiga jumla ya mechi zaidi ya tatu za ligi hiyo ya Seria A, Italia. Messi akiongelea kuondoka kwa Ronaldo pale Real Madrid: “Real Madrid ni moja ya timu kubwa duniani na wana kikosi poa [lakini] kukosekana kwa Ronaldo kunawapunguzia wakali na kuifanya Juventus kuwa [moja ya] timu itakayoshinda Champions League.


Povel tz
Gud news