Kila mchezo una maajabu yake! Haikutarajiwa! Ni kwamba mshindi mara 20 wa Grand Slam kutoka Uswisi, Rodger Federer amejikuta yupo nje ya michuano ya Us Open! Hii ni mara baada ya yeye kutolewa na John Millman ambaye ni mchezaji namba 55 kwenye tenisi ubora duniani.
Tofauti na matarajio ya wengi
Mashabiki wote, kila mtu, waliamini kuwa Federer akicheza na Millman basi itakuwa ni moja ya mechi rahisi kwake ila mashabiki waliokuwa wamekusanyika viwanja vya Flushing Meadows walishangazwa sana na matokeo ya mwisho wa mtanange huo!
Ushindi wa 3-6 7-5 7-6 7-6 katika muda wa masaa 3 na dakika 35 ulishuhudia Federer akitolewa ambapo imekuwa ni mara ya kwanza kwake kutolewa kwenye michuano hiyo mikubwa na mchezaji ambaye hayuko hata kwenye 50 bora duniani.
Takwimu zake
Federer, Kwenye mechi 41 zilizopita, hajawahi kabisa kufungwa na mchezaji aliye nje ya 50 ya juu na Millman mwenyewe amekiri kwamba haamini alichofanya kutokana na heshima kubwa aliyonayo kwa Federer kama mchezaji mahiri.

Djokovic anabamba!
Kwenye mtanange mwingine Novack Djokovick naye amekwenda hatua ya robo fainali baada ya kuibuka kidedea kwenye mechi yake akicheza na Joao Sousa.
Huyu Djokovick ni bingwa mara 2 wa michuano hiyo. Aliweza kushinda mchezo huo kwa jumla ya seti 6-3 6-4 na 6-3 na kwa ushindi huu sasa Djokovick anakwenda kukutana na John Millman! Patamu hapo!



aisha
hongera kwake