Diego Costa Amejitoa Kwenye Kikosi Cha Taifa

Straika wa Uhispania, Diego Costa amejitoa katika kikosi cha taifa cha Hispania kinachoenda kucheza katika Ligi ya Mataifa -Uefa dhidi ya Croatia na Uingereza kwa sababu zake binafsi. Taarifa Kutoka Shirikisho la Soka Hispania kinaripoti kuwa nafasi ya Costa itazibwa Iago Aspas mwenye umri wa miaka 31 kutoka Celta Vigo.

Diego atakosa kuitumikia timu yake ya taifa ya Uhispania inapokwenda kuchuana na Uingereza kwenye dimba la Wembley ikiwa ni mechi ya kwanza chini ya kocha Luis Enrique aliyewahi kuwa meneja wa Barcelona toka mwaka 2014-2017.

Kikosi cha Enrique kinawajumuisha wachezaji wa 4 kutoka Barcelona ambao ni Marcos Alonso, Alvaro Morata, Cesar Azpilicueta na Kepa Arrizabalaga. Golikipa wa Real Betis Pau Lopez, Beki wa Valencia Jose Gaya na kiungo wa Real Madrid Dani Ceballos wote wapo katika kikosi cha bwana Enrique.

Kikosi kizima cha Hispania

Magolikipa: David de Gea (Manchester United), Kepa Arrizabalaga (Chelsea), Pau Lopez (Betis)

Walinzi: Dani Carvajal (Real Madrid), Nacho (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Diego Llorente (Real Sociedad), Inigo Martinez (Athletic Bilbao), Jose Gaya (Valencia), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Marcos Alonso (Chelsea), Raul Albiol (Napoli)

Viungo: Sergio Busquets (Barcelona), Sergi Roberto (Barcelona), Rodri (Atletico Madrid), Saul Niguez (Atletico Madrid), Dani Ceballos (Real Madrid), Thiago Alcantara (Bayern Munich)

Washambuliaji: Isco (Real Madrid), Marco Asensio (Real Madrid), Iago Aspas (Celta Vigo), Rodrigo Moreno (Valencia), Alvaro Morata (Chelsea), Suso (AC Milan)

3 Komentara

    Hana lolote huyo,kwanza nizamu hana.

    Jibu

    Anazinguaga

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.