Straika wa Monaco Muitalia Pietro Pellegri amechomolewa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia katika mechi mbili zijazo. Pietro Pellegri alipata wito katika kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kupambana na Poland na Portugal.
Taarifa kutoka shirikisho la soka la timu hiyo FIGC iliyowekwa katika tovuti ya shirikisho hilo imeonyesha kikosi cha italia tayari kimeshaanza mazoezi bila ya Pellegri ambaye ametakiwa kurudi katika klabu yake kufuatia vipimo vinavyoonyesha hana hali nzuri kwa sasa.
Timu ya kandanda ya Italia itamkaribisha Poland kabla hawajasafiri kwenda kumenyana na Portugal siku tatu baadae. Timu ya Italia imekubaliana na Monaco kuwa Pellegri atarejea hospitali kupata matibabu ya majeraha yake.


Povel
Duh majanga kwl