Namba za Jezi Zilizowekwa Kabatini

Kuna historia ambayo mara nyingi hujificha ndani ya jezi fulani zinazovaliwa na wachezaji wa klabu mbalimbali wanazozichezea. Baadhi ya namba huwa na maana kubwa kwa wachezaji wanaozitumia. Bayern Munich wao waliwapa heshima mashabiki zao kwa kuwapa jezi namba 12, lakini klabu nyingine hufanya hivyo kutokana na tukio fulani lililowahi kumtokea mchezaji akiwa ndani ya jezi yenye namba hiyo.

Barcelona (Na. 21)

Klabu hiyo iliamua kuifungia jezi hiyo yenye namba 21 ambayo ilikuwa ikivaliwa na kocha aliyehudumu ndani ya klabu hiyo kwa kipindi kirefu na kuipa mafanikio, Luis Enrique. Kwa sheria zao hawana utaratibu wa kuifungia namba ya jezi lakini kutokana na kupata wakati mgumu kumpata mchezaji wa aina yake walifikia maamuzi hayo magumu.

Pachuca (Na. 8)

Kutokana na mchango ndani ya klabu hiyo, Gabriel Caballero pamoja na kucheza klabu sita tofauti mchezaji huyo alipewa heshima kubwa katika klabu yake hasa ile ya kuihifadhi namba ya jezi yake isiweze kutumiwa kwa kipindi fulani ikiwa kama hatua ya kuuenzi msaada wake na makubwa aliyoyafanya. Vazi lake hilo liliweza kuhifadhiwa kwa kipindi cha miaka mitano na baadaey kuachwa Hirving Lozano akapewa tena.

Schalke 04 & Stabæk (Na. 7)

Schalke 04 waliacha matumizi ya jezi yenye namba hiyo kama sehemu ya kumuenzi na kumtunuku mchezaji wao Raul ambaye alikuwa raia wa Hispania kutokana na sababu kwamba ilikuwa ni vigumu kwao kupata mbadala wa aina yake katika kikosi chao. Japo baadaye walilegeza maamuzi yao na kumpa jezi hiyo Max Meyer anayeonekana kuitendea vyema kabisa. Pia Stabæk walifanya maamuzi ya kuifungia namba ya vazi hilo hadi leo ikiwa ni hatua ya kumpa heshima Christer Basma aliyekuwa mlinzi wao baada ya kustaafu.

AS Roma (Na. 6)

Raia wa Brazil aliyekipiga ndani ya klabu hiyo, Aldair alikuwa akiivaa jezi hiyo na baada ya kustaafu kucheza soka ilibidi apewe heshima ya pekee kwa kuitunza namba yake kihistoria ili kumpa heshima yake. Mlinzi huyo wa kati alitakiwa kuwa kapteni wa klabu yake lakini alipendekeza kwamba Totti aliyekuwa na umri wa miaka 22 wakati ule angefaa kwa nafasi hiyo lakini kadri wakati ulivyozidi kwenda mchezaji huyo aliamua kuruhusu jezi hiyo irudi uwanjani tena baada ya Kevin Strootman kuomba kuitumia upya.

Faida ya kuyafanya haya

Utamaduni wa aina hii huchochea wachezaji kuzipenda klabu zao na kuzipigania ili kuweza kujenga heshima ya aina hii yenye lengo la kuchagiza ushindani ndani na nje ya uwanja kwa wake wanaochipukia katika soka.

3 Komentara

    Iko poa.

    Jibu

    Utamaduni wa aina hii huchochea wachezaji kuzipenda klabu zao

    Jibu

    Duh habar njema

    Jibu

Acha ujumbe