Klabu ya manchester united imethibitisha kuwa aliyekuwa meneja wa klabu hiyo, Alex Ferguson ataiongoza klabu hiyo kwenye mechi ya muhimu ya kumbukumbu pale Old Trafford mwezi Mei. Unashangazwa na mkongwe huyu kurejea United?
Meneja huyu wa zamani wa klabu hii alistaafu mwaka 2013 baada ya kuwaongoza mashetani wekundu kuutwaa ubingwa wao wa 20 wa Ligi yaUingereza ikiwa ni mara ya mwisho tokea walipoupata ubingwa huo.
Mzee huyu amepata mafanikio makubwa katika miaka yake 27 klabuni hapo kwenye Premier League, Champions League na FA Cup mwaka 1999.
Man U wanatarajia kucheza gemu ya kumbukumbu dhidi ya Bayern Munich Mei 26, gemu hii itatumika kutengeneza kipato cha Manchester United Foundation. Ferguson ataiongoza Man U ambao watakuwa nyumbani kwenye gemu hiyo.


Antony Luseno
Old is gold,muda wote sir man united inamhitaji
Issa
Ataleta hamasa united
Furahav
Itakuwa hatari.
Povel
Gud news