Winga wa Man city Leroy Sane mwenye umri wa miaka 22 ameshauriwa kubadili tabia yake ili aweze kupata nafasi na kufanya vizuri. Sane alijiunga na Man City mwaka 2016 akitokea Schalke 04, alitemwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia lakini amepata nafasi ya kurejeshwa katika kikosi kwa ajili ya michuano ya UEFA kinachoenda kucheza na Ufaransa kabla ya kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Peru.
Leroy Sane bado hajapata nafasi kucheza katika kikosi cha Man City, na alitemwa katika kikosi cha Jumamosi kwenye gemu dhidi ya Newcastle United waliyopata ushindi kwa bao 2-1. Mchezaji mwenzie kwenye timu ya taifa ya Ujerumani, Toni Kroos ambaye ni kiungo wa klabu ya Real Madrid anasema “hauwezi kumuelewa vyema sane kwa wakati wowote, hata tukiwa tumeshinda au tumeshindwa yeye huwa na ishara zilezile”
Lakini Sane alishinda tuzo ya mchezaji chipukizi wa mwaka 2017/2018 akiwa amefunga magoli 10, na pasi 15 za magoli msimu uliopita wa Premier League. Staa huyu anadaiwa kuwa licha ya kuwa mchezaji mwenye uwezo mzuri bado kuna wakati anahitajika kusisitizwa aonyeshe uwezo wake wa juu zaidi ili afanye vizuri. Huenda akifanya vyema na kuonyesha nidhamu zaidi atapata nafasi mara nyingi zaidi za kuonyesha ubora wake.


Povel
Gud new