Nondo Za Rangnick Kabla ya Brentford.

Wanamuita Profesa wa mchongo, Ralf Rangnick anapambana na kibarua kigumu kule Old Trafford. Hizi ndio nondo zake kuelekea mchezo dhidi ya Brentford wiki hii.

Manchester United watacheza dhidi ya Brentford kwa mara ya kwanza toka mwaka 1975 wakati timu hizi zilipochuana kwenye mchezo wa mashindano. Timu zote zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa zimetoka kwenye maumivu.

United alishindwa kufurukuta na kuondoka na pointi 3 kule Villa Park huku Brentford akiambulia kipigo kule Anfield. Ralf Rangnick atakuja na nini safari hii?

Katika nondo za Rangnick mchana huu, amegusia hali ya kikosi chake ambapo, CR7 na Rashford wanaweza kuwepo kwenye kikosi kesho usiku (itategemea na maendeleo yao kwenye mazoezi). Pogba amerejea kwenye mazoezi lakini, ataendelea kuwa nje kwa wiki 1 au 2 zaidi.

Nondo

Kuhusu sakata la Anthony Martial, Rangnick ameeleza kuwa;

Nilizungumza na Anthony (jumapili), maongezi yalikuwa ni kati yetu wawili na nilimueleza nilichokiona. Hilo limeisha kwa sasa, tutaona mambo mengine yatakavyokuwa.

Vipi kuhusu mchakato wa mkataba wa Paul Pogba? Ralf anasema;

Sihusiki moja kwa moja na mikataba ya wachezaji lakini, toka aliporejea jana kwenye mazoezi (kwa mara ya kwanza), unachoweza kukiona ni uwepo wake. Uwepo kwa maana ya mwili na akili yake. Nilichokiona ni hamasa njema kwa siku zijazo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe