Ronaldo Awajibu Wanaouliza Atastaafu Lini

Mshambuliaji wa timu ya Ureno na Manchester United Ronaldo ameeleza ni muda gani anatarajia kuendelea kucheza alipohuzulia hafla ya tuzo za FIFA.

Ronaldo alifanikiwa kutunukiwa tuzo maalumu ya FIFA kwenye sherehe hizo baada ya kuvunja rekodi ya ufungaji kwenye michezo ya kimataifa akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno mwaka 2021 akifunga magoli 115.

Sherehe hizo ilikuwa kama sehemu ambayo aliweza kuelezea ni kwa miaka mingapi zaidi ataendelea kucheza mpira, na pia alikubali kuwa anaulizwa mara kwa mara kua atastaafu lini, aliamua kulielezea hili swala kama kuwajibu wale wanaomuuliza.

Kila ninapokwenda uwanjani, hata mazoezini, nafarijika sana hamasa yangu bado ipo hapo  hata kama nakaribia miaka 37.

“Najisikia vizuri, najisikia kuhamasika. Nimeanza kufanya kazi kwa juhudi tangu nikiwa na miaka 18, bado naupenda huu mchezo, bado nina hisia nao na nahitaji kuendelea.

“Watu wananiuliza ni miaka mingapi zaidi nitaendelea kucheza, na nawaambia nitacheza kwa miaka minne, miaka mitano au zaidi.

“Ni swala la kuwa vizuri kiakili sababu mwili ukiutunza vizuri , utakupa kusaidia pale utakapohitaji kuutumia.” Alieleza Ronaldo


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe