Ozil ambae alikua kiungo wa zamani wa Arsenal  ametuma ujumbe wa kumuunga mkono nahodha wa Manchester United Harry Maguire baada ya kupokea tishio la bomu.

Maguire amepokea vitisho vya bomu kufuatia kupoteza kwa United 4-0 kwenye uwanja wa Anfield Jumanne usiku.

Polisi wa Cheshire wamesema kwamba maafisa wamefika nyumbani kwa mchezaji huyo wa Uingereza, ambapo anaishi na mchumba wake Fern Hawkins na binti zake wawili.

Ozil ameandika kwenye akaunti yake ya Tweeter,

“Kandanda kamwe haiwezi kuwa mbaya kiasi hicho cha kutishia mchezaji na familia yake. Ninashangaa. Wakati mwingine soka huleta hali mbaya zaidi kwa watu. Tunatumahi, watu wote wanaohusika wataadhibiwa.”

Mesut Ozil
Mesut Ozil

Maguire alisajiliwa na United kutoka Leicester City mnamo Agosti 2019 kwa ada iliyoripotiwa ya £80m.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa