Baada ya kutangazwa rasmi kama kocha mkuu wa Manchester United, Erik Ten Hag atapeleka genge la kiholanzi kwenye EPL?

Ten Hag anatua United kwa mkataba wa miaka 3 wenye uwezakano wa kuongeza mwaka 1 zaidi. Kuingia kwa Erik kwenye usukani wa Man United, huenda ukafungua njia kwa wachezaji wakiholanzi kucheza EPL na hasa Manchester United?

Ni wachezaji wachache wa taifa hilo ambao wamefanikiwa kucheza EPL na wakawa na mafanikio makubwa. Kizazi kile kimeshapita na sasa kuna damu changa kwenye soka la nchi hiyo. Baadhi yao walipita mikononi mwa Ten Hag akiwa anaiongoza Ajax kwa takribani miaka 5.

Van De Beek, Frankie De Jong, De Ligt, Gravenbach na wengine, ni baadhi ya majina ya wachezaji walionolewa vyema na kocha huyu. Tayari Van De Beek yupo United. Japokuwa hajawa na nyakati nzuri nchini Uingereza, pengine huu ndio muda wake.

Ten Hag, Ten Hag Kupeleka Uholanzi EPL?, Meridianbet
Wakati De Jong (kushoto) akiwa na De Ligt (kulia) walipokua wanaitumikia Ajax.

Uwepo wa Ten Hag ndani ya Manchester United kuanzia Juni 1, 2022 huenda ukawa ni mchongo kwa baadhi ya wachezaji nyota aliowahi kuwafundisha? De Jong na Athony ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa na United baada ya ujio wa Erik. Hawa ni wachezaji wawili wenye uwezo mkubwa uwanjani (kwenye nafasi zao) na pia, wamekua muhimili mkubwa kwenye kikosi cha timu yake kwa nyakati tofauti tofauti.

Pamoja na wachezaji, huenda Erik akatua United na baadhi ya wataalamu wa michezo kutoka Uholanzi ambao kwa pamoja, watasaidiana nae kuiendesha Manchester United kwa muda atakaokuepo Old Trafford.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa