Yanga Inakimbiza kwenye ligi. Ikiongoza kwa point 10 juu ya mtani wake Simba. Yes! Kwa magoli, pointi, pasi, mashuti, ubora wa mchezaji mmoja mmoja, asilimia kubwa wapo juu zaidi.

Lakini kuna maeneo matatu yanahitaji tiba, kwa ligi ya mabingwa mwakani watazingua. Pale golini anahitajika mtu zaidi. Kimo cha yule Diarra ni kitendawili sana, hili pia ni gonjwa kwa Yanga.

Anafanya vyema ni kipa wa kisasa sana na huanzisha mashambulizi mara kadhaa, akitumia vizuri miguu yake na kuitazama mechi kwa jicho kali. Pia ni mwepesi wa kuongea na mabeki. Ila kile kimo, hapana.

Upande wa beki tatu hakuna mwenye uhakika. Siyo uhakika wa namba bali wa kuwapa amani ya moyoni Wananchi. Yassin, Faridi Mussa na Bryson wako nyuma ya Mohamed Hussein.

Yanga
Yanga

Ugonjwa mwingine ni pale juu. Mayele katawala kiasi cha kukosa msaidizi sahihi. Akipata majeruhi au wakitaka kutumia washambuliaji wawili, Yanga watasota sana.

Mayele ni noma. Ugonjwa huu utibiwe fasta sana. Kutupia goli ni kazi ngumu kuliko yoyote uwanjani. Lazima apate pacha sahihi, kwani Makambo ukweli kachemka kabisa.

Kumbuka Mayele angekuwa Simba, mpaka sasa angekuwa na goli hata 50. Simba hutengeneza nafasi nyingi sana lakini hawazitumii, Mayele anatumia kila nafasi, lakini Yanga hawatengenezi nafasi za kutosha.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa