Juni 17 huenda ikawa ni tarehe ya kumbukumbu kwenye maisha ya Paul Pogba. 2022/23 huenda ikaanzia hapo.

Ni rasmi kuwa Pogba na Man United wameshamalizana baada ya miaka 6. Ukilisikia jina lake, ni vilabu viwili tu vinakujia kichwani – United na Juventus. Ubora wake ulionekana kwenye vilabu hivi pekee.

Amekuzwa kwenye mfumo wa vijana wa Man United kabla ya kuondoka kama mchezaji huru mwaka 2012. Alipotua Juventus alikua ni moto wa aina yake kabla ya kuuzwa na kurejea tena United kwa dau kubwa lililoweka historia wakati ule. Unaikumbuka “Pogback”? Hajawahi kuishiwa namna za kuiteka dunia.

Maisha ndani ya United yakawa ya misukosuko, mivutano na kila aina ya rabsha. Hakika, mbio za sakafuni huishia ukingoni. Miaka 6 imekatika na sasa anaondoka Old Trafford kama mchezaji huru, Manchester United wanaikosa faida ya usajili wa Paul kwa mara ya pili.

Pogba, Pogba: Juni 17, 2022 Tutatokaje?, Meridianbet
Usajili wa Paul akitokea Man United, 2012.

Sekeseke la Paul limeanza muda mrefu hata kabla ya wakala wake -Mino Raiola kufariki dunia. PSG, Real Madrid na Man City zote zimeshahusishwa sana na usajili wake. Madrid sababu kubwa ilikua ni Zidane huku PSG akiwa ni Leonardo ndiye aliyemuhitaji. Hawa wote hawapotena kwenye vilabu hivi.

2016 kabla hajarejea United, Paul aliweka wazi heshima na namna anavyopendezwa na uongozi wa Pep Guardiola. Wakati huo ndio kwanza Pep alikua ametua Etihad. 2021/22 City wanauhusishwa na Pogba halafu, Paul anaikataa City mchana kweupe.

Pogba, Pogba: Juni 17, 2022 Tutatokaje?, Meridianbet
Usajili wa Paul akitokea Juventus, 2016.

Yote 9, mchongo upo hivi. Paul yupo kwenye mchakato wa kutoa filamu ya maisha yake ambapo, filamu hii inatajwa huenda ikawekwa sokoni mwezi Juni mwaka huu. Wakati huohuo, tetesi zinasema huenda Juni 17, ikawa ndio siku ambayo, Juventus itamtangaza rasmi Paul kama mchezaji wao kwa kandarasi ya miaka 4. Ikumbukwe, hii itakua ni mara ya pili kwa mchezaji huyu kurejea Allianz Stadium akitokea Man United, anarudi nyumbani.

Kwa matukio haya mawili, Juni 17 huenda ikawa ni siku muhimu kwenye maisha ya Paul Pogba ambapo, atakwenda kuusimamisha ulimwengu wa soka kwa muda ili kufanikisha jambo lake adhimu. Itakua hivi, au ni akili za muandishi?


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa