Rhine na Ruhr- ilivyobeba historia ya vilabu vikubwa Bundesliga

Sauti za wapenda soka zinaulizana mbona huyu Mesuit Mostafa Ozil fundi sana, mbona Marco Reus mtu sana, vipi kuhusu Mario Gotze ‘Computer’? yule Sammy Khedira je? Watu wanamtaja na Manuel Neuer, Julian Draxler ila mimi namkumbuka Hans Gunter Bruns ‘ufagio’.

historia ya Ruhr Region huko Ujerumani Magharibi ilianzia karne ya 18 baa da ya Waingereza kuhamia nchini humo, soka likaanza kupigwa sana, eneo hilo ni la viwanda vingi hivyo wafanyakazi na watoto wa Kijerumani wakaanza kulisakata na wao. Rhine na Ruhr ni mito miwili mikubwa eneo hilo, ila kuna klabu nne kubwa, Schalke 04, Borrusia Dortmund, Borrusia Monchengladbach, Cologne, mechi kati ya Monchengladbach na Cologne ndio derby ila Dortmund na Schalke ni Local.

Taarifa rasmi zinadai Ruhl ndio sehemu pekee duniani soka lina ukichaa wake, mashabiki wa Schalke 04 wanaoana wenyewe, wana kanisa lao la kusali na wana sehemu ya kuzikia,  hizo siasa zinasimamiwa na kundi la Schalker Knappen hawa ni wachimba madini ya ukaa

Unapofika Dortmund ndani ya Signal Iduna Park, wenyewe wanakwambia ile ni Temple ya soka, huwezi kusema wewe ni muumini wa soka kama hujaenda kusali Iduna Park, Mashabiki wa Ujerumani huwa wanashangilia kwa kutengeneza ukuta wanaita Yellow wall,

Hapa Iduna ndio uwanja pekee wenye sehemu kubwa ya kusimama, hawataki ukae ili kiwe nini? Hapo Iduna shabiki ndie mtangazaji wa mechi, inaaminika matangazo ya redio ni ngumu sana kusikika.

2 Komentara

    Wote wanajua sana.

    Jibu

    Habari njema Sana Asante kwa taarifa meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe