Zamani sana Jijini Milan nchini Italia miaka 16 iliopita kulikuwa na jina la Playmaker mmoja mstaarabu mno, muungwana kutoka Mji wa vipaji wa Sao Paulo nchini Brazil.
Ricardo Izecson dos Santos Leite ‘Kakà’ Nani asiyemkumbuka fundi huyu ambaye anatua uwanja wa ndege wa Malpensa kwenye kitongoji cha Varese pale Italia na biblia yake, Waitaliano wanamtazama Silvio Berlusconi na Carlo Ancelotti, nyie vipi mnatuletea mtoto laini huyu, ataweza kweli soka la Italia, ataweza kweli kupasua Catenacio na Uchawi mweusi kwenye kujilinda?

Maswali yalikuwa mengi ila Kakà alijibu juu ya nyasi za San Siro, aliwapa majibu mashabiki kindaki ndaki wa Milano, Fossa de Leoni kundi la mashabiki lilofunguliwa mwaka 1968 japo 2005 lilisambaratika, hawa walivua kofia kwa Mbrazil huyu ambaye hakuwa na mambo mengi kwenye kazi yake lakini kila kitu alichofanya kilifana.
Ancelotti aliamini Kaka anafaa kuungana na Andriy Shevchenko na Philpo Pippo Inzaghi kwenye eneo la mwisho, Carlo aliamini miguu ya Manuel Costa na akili yake haiwezi tena kufanya hata nusu ya ubora wa Kakà, fundi huyo alitengeneza nafasi kiasi kwamba pale kati kila kitu kilikuwa moto

Kule nchini kwao Brazil ilimlazimu Kocha wa timu ya taifa ajifungie kwenye office za CBF, kufikiria anamtumiaje Ricardo kwenye mfumo wake, Carlos Alberto Pereirra alikuja na 4-2-2-2 ili awe tu na fundi wa Sao Paulokwenye kikosi chake
Kumbuka una namba 9 ya Ronaldo De Lima, una namba 10 ya Dinho Gaucho kisha una straika mwingine mwenye mnuso wa bundi kama Adriano, kazi ya Kakà ilikuwa ni kuunganisha, kupikia na kuwafanya wawe free kule mbele, ikumbukwe hakuwa mchoyo
Kiungo chake kilikuwa sio cha kupiga pass tu, bali kuhakikisha imefika tena kwa mlengwa, kiungo chake hakikuwa cha kuwachezesha tu mastraika bali kuhakikisha amewarahisishia kila kitu, alikuwa mwepesi kwenye kupunguza mabeki.
Utasema nini kuhusu ucha Mungu wake? Wakati Pato anaenda Milano aliwahi kuulizwa na De Lima, unamfata Kakà au Mimi, yani unataka maisha ya dini au maisha ya bata De Lima alitaka kumpa jarida la Playboy kijana Pato.


Rehema
Asante kwa taarifa
Ester jackson
Aaah hakika kwel kabisaa
Furahav
Habari poa
Issa
Kiungo makini