Veterani anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich Arjen Robben anasema kwa mtazamo wake Anfield ndiyo dimba baya zaidi kwake wakati wakifanya maandalizi kuelekea kwenye gemu na Liverpool dimbani hapo.
Mabingwa hawa wa Bundesliga wanatarajia kusafiri kwa ajili ya gemu ya Ligi ya Mabingwa mzungukuko wa timu 16 dhidi ya watabe wanaokimbiza Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu Jumanne hii.

Nyota huyu ambaye pia anatarajiwa kusepa Bayern mwisho wa msimu anaripotiwa kuwa alikuwa na nyakati mbaya sana kwenye dimba hilo wakati alipokuwa aklichezea Chelsea.
Chelsea walitandikwa na Liverpool bao 1-0 kwenye nusu fainali za Ligi ya Mabingwa mwaka 2004-05. Pia, mwaka 2006-007 walichapwa tena kwenye hatua hii hii ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati. Liverpool walikuwa wakiwaonea dimbani hapo.
“Nafikiri nikizungumzia uwanja ambao ni mbaya zaidi kwangu, nafikiri ni uwanja wa Liverpool. -Arjen Robben


Furahav
Uko sahii.