Juve Kwenye Orodha ya Wamiliki Matajiri

Klabu ya Juventus ipo kwenye orodha ya klabu ambazo zinamilikiwa na wamiliki matajiri zaidi. Klabu hii inashikilia nafasi ya 3 kwenye chati wakati wapinzani wao Inter Milan wakiwa nafasi ya 9.

Familia ya Agnelli ambao ndio wamiliki wa klabu hii wanajumla ya utajiri unaofikia paundi bilioni 10.4 na kuwafanya Juventus kuwa vinara kwa upande wa Serie A.

Inter Milan ambao wapo nafasi ya 9, wanamilikiwa na kikundi cha Sunning -Sunning Group ambachjo mmiliki mkuu Zhang Jindong ana utajiri binafsi wa paundi bilioni 5.2, wanakuwa mbele ya Tottenham wanaokamatia nafasi ya 9.

Klabu ambayo mmiliki wake ana pesa zaidi ni klabu ya Red Bull Salzburg na RB Leipzig ambazo mimiliki wake Dietmar Mateschitz ana utajiri wa paundi bilioni 17.8.

Orodha ya 10 bora ya wamiliki matajiri zaidi.

1. Dietmar Mateschitz (Red Bull Salzburg/RB Leipzig, £17.8bn)
2. Sheikh Mansour (Manchester City/City Football Group, £17bn)
3. Agnelli family (Juventus, £10.4bn)
4. Philip Anschutz (LA Galaxy, £10bn)
5. Roman Abramovich (Chelsea, £8.3bn)
6. Stan Kroenke (Arsenal, £6.4bn)
7. Nasser Al-Khelaifi (Paris Saint-Germain, £6.2bn)
8. Shahid Khan (Fulham, £5.4bn)
9. Zhang Jindong (Inter/Jiangsu Suning, £5.2bn)
10. Joe Lewis (Tottenham Hotspur, £3.8bn)

3 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Hatari sana hii.

    Jibu

    Hii noma

    Jibu

Acha ujumbe