Prince Amekanusha Kuinunua United

Kulikuwa na taarifa kuwa mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Prince Mohammed Bin Salman kuwa anahitaji kuinunua klabu ya Manchester United na yupo mazungumzoni kukamilisha dili hilo kwa ofa ya paundi bilioni 3.8.

Hata hivyo baadhi ya ripoti pia zilidai kuwa Glazers hawana mpango wa kuiuza klabu hiyo ambayo waliinunua mwaka 2005 kwa paundi milioni 790.

Waziri wa habari wa Prince Mohammed Bin Salman amekanusha uvumi huu na kusema kuwa ni kweli klabu hiyo ilikuwa kwenye kikao na kitengo cha Uwekezji wa Umma (Public Investment Fund) kwa ajiri ya kujadili fursa ya ufadhili. Hakuna dili ambalo limefanyika.

Prince Mohammed Bin Salman aliteuliwa kuwa Crown Prince mwaka 2017 akitarajiwa kurithi kiti cha ufalme cha nchi hiyo.

Nchi hiyo inatuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu kufuatia kifo cha Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi katika ubalozi wa Saudi Arabia mwaka Jana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.