Baada ya mechi kadhaa kupigwa wiki lililopita leo michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inarejea tena viwanjani kwa mitanange mikali inayotegemewa kuwa na ushindani wa kusisimua sana kitu ambacho kila mpenda soka duniani anaamini kushuhudia mechi zenye ushindani wa hali ya juu na wenye kuvutia kutoka kwa wapinzani hao wanaoangaliwa kwa jicho la pekee duniani kutokana na uwezo wa vikosi vyao siku za usoni.
Mechi hizo zinazotegemewa kuanza kushika kasi saa 11.00 kwa saa za Afrika Mashariki zitashuhudia Liverpool akiingia uwanjani kukabiliana na mabingwa wa ligi ya Ujerumani, Bayern Munich ambao hawajawa na msimu mzuri bado katika ligi yao. Hicho ni miongoni mwa vitu vinavyowapa imani Liverpool ambao wamekuwa vizuri sana katika misimu hii miwili chini ya Klopp.
Mbali na kuwaamini huko ikumbukwe Majogoo hao watakuwa uwanjani leo huku wakiwakosa baadhi ya nyota wao tegemezi ndani ya kikosi hicho ambao ni Van Dijk aliyepata kadi nyekundu katika michuano hiyo kwenye mechi za awali. Hivyo safu yao ya ulinzi itakuwa bila mchezaji huyo ambaye amekuwa nguzo kubwa na muhimili mkubwa kwa sasa ndani ya himaya hiyo kuhakikisha ulinzi unakuwa salama.
Pia wapo wachezaji wengine ambao kutokana na afya zao wanaweza wasionekane uwanjani leo na kukaa kushuhudia kile kinachofanywa na wenzao tu kama vile Gomez, Lovren, Chamberlain na Shaqiri ambaye anaonekana kuanza kurejea kwenye hali yake ya kawaida kiafya baada ya kuwa nje kwa kipindi fulani.
Upande wa mpinzani wake, Bayern Munich yupo hatihati katika mchezo wa leo kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota wa muhimu ndani ya kikosi chake akiwemo Muller anayetumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata siku za usoni; pia wachezaji wengine tegemezi ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa nje ya mchezo ni kama Robben, Tolisso na mlinzi wao Boateng.
Gemu nyingine
Mechi nyingine itakayopigwa ni kati ya miamba wa Uhispania, Barcelona atakayekuwa ugenini dhidi ya Wafaransa Lyon. Wawili hao wanategemewa kuonesha soka safi japo kuna walakini endapo mwenyeji huyo ataweza kutamba katika uwanja wake wa nyumbani. Japo hapewi nafasi kubwa mbele ya mchwa hao wenye kawaida ya kutafuna chochote kinachoonekana kuwa halali kwao.
Vikosi na utabiri
Kwa upande wa vikosi vijana hao wa Genesio watakuwa uwanjani huku wakimkosa nyota wao Nabir Fekir anayekula kadi nyekundu, Ndiaye ambaye yupo majeruhi lakini upande wa pili kwa aina ya kikosi chao kila mchezaji ana uwezo wa kuleta matokeo akipata nafasi japo wanawakosa nyota wao kama Rafinha atakayekuwa nje kwa msimu mzima, Arthur pia Cillessen ambao ni vigumu kuonekana katika mechi yao ya leo. Kutokana na uchambuzi huo mechi ya Liverpool ni 60/40 na ile ya Lyon ni 30/70.


Povel
Don’t miss
Lydia Emmanuel Magoti
Iko vizuri