Baada ya mechi za awali kupigwa na matokeo kupatikana hatua inayoelekea kwa sasa ni robo fainali ambapo timu hizo zitaumana tena ili kupata timu zitakazoelekea hatua ya nusu fainali. Ndani ya michuano hiyo timu kubwa zilizofanikiwa kupenya kusonga mbele ni zile zinazotoka jiji la Manchester ambazo ni United na City.
United amesonga mbele baada ya kumfunga Chelsea aliyekuwa uwanja wa nyumbani. Chelsea ambayo kwa sasa inaonekana kutokuwa na mwelekeo unaoeleweka kwa sasa walikubali kichapo hicho; mbele ya vijana kutoka jiji la Manchester baada ya kuonesha mapungufu makubwa katika kipindi cha kwanza. Katika hatua hiyo inayofuata, United ataumana na Wolves katika hatua ya kuelekea nusu fainali na anapewa nafasi ya kusonga zaidi mbele katika michuano hiyo.
City wao walipewa timu ambayo haikuwatoa jasho kwa kiasi kikubwa, Newport Country baada ya kuwaadabisha goli 4-1 wakiwa ugenini. Mechi hiyo ilionekana kuelemea upande kutokana na uimara wa kikosi cha City kwa siku za karibuni na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wakiwa uwanjani, hicho kinawapa nguvu sana. Kwa sasa atakutana na watoto wa mjini, Swansea City ambapo bila wasiwasi atafanya vizuri katika nafasi hiyo.
Wengineo wamepangwa vipi?
Watford atakuwa na kibarua kigumu mbele ya Crystal Palace ambao wameweza kupenya katika hatua hiyo baada ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao; ambapo Palace aliweza kumfunga Doncaster akiwa ugenini. Pia, Watford alishinda mbele ya QPR kwa goli 1-0 katika mchezo uliokuwa wa kuvutia wakati wote.
Millwall atakuwa mwenyeji wa Brighton katika hatua ya robo fainali ndani ya michuano hiyo ambayo kwa nafasi yake inaonekana kuwa ni yenye kuvutia sana. Millwall amepenya baada ya kupata ushindi mbele ya Wimbledon, wakati huo mpinzani wake anayeenda kukutana naye alipenya baada ya kupata ushindi wake mbele ya Derby Country waliokuwa na matumaini makubwa kusonga mbele.
Wanaopigiwa upatu zaidi
Baada ya matokeo hayo timu zinazowekewa jicho pevu kukutana katika hatua inayofuata ni United na City kutokana na aina ya vikosi vyao na matokeo yao ya hivi karibuni kitu ambacho kinaweza kisizuilike kwao kukutana katika hatua inayofuata. Hii itakuwa nafasi na mafanikio makubwa kwa United ambayo ingeweza kumaliza msimu bila kuwa na kikombe chochote.
Pamoja na hilo bado kuna walakini kwa sababu katika hatua ya robo fainali zitapatikana timu nne ambazo zitatakiwa tena kukutana ili kupata wawakilishi wawili. Hivyo basi endapo wawili hao watakutana hatua ya nusu fainali haiwezi kushuhudiwa fainali ya wawili hao bali fainali yao itakuwa katika hatua ya nusu fainali. Ni furaha ya kila mpenda soka kuona wawilli hao wanakutana katika fainali ili kushuhudia kandanda safi kati yao.


Povel
Habar njema