Mwanasoka Alexis Sanchez ametoa msisitizo kwamba yeye atazimudu changamoto zinazomzunguka kuhusiana na kiwango chake na kuwa atakuwa staa pale Manchester United anakokipiga kwa sasa.
Mchezaji winga huyo wa Chile ana umri wa miaka 29 kwa sasa na amekuwa na maisha magumu sana pale Old Trafford tangu aliposajiliwa mwezi wa kwanza.
Mpaka sasa hajaweza kufanya lolote la msingi sana ambalo linalingana na thamani ya mshahara wake wa paundi 500,000 kwa juma kwani amepachika bao 1 pekee kwenye gemu 10 alizokipiga.
Hata hivyo Sanchez amedai kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu kwake na kuwa shinikizo na ukosolewaji unaomuandama ndiyo unampa nguvu.


Issa
Sanchez ni hodari mazingira ndio yanamsumbua tu
Povel
Sanchez mwamba
farida ahmadi
Habari njema Sana