Winga wa Man City Leroy Sane ametangaza kupata mtoto wa kike ikiwa ni siku moja baada ya kuondoka katika kikosi cha timu ya ya taifa ya Ujerumani. Staa huyu aliripotiwa kuondoka jana katika hoteli za ya timu ya taifa ya Ujerumani kwa sababu zake binafsi, sababu hiyo ilikuwa ni mkewe aliyekuwa mjamzito.
Taarifa zilidai kuwa sane hatakuwepo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Peru jumapili hii baada ya mazungumzo na kocha mkuu Joachim Low.
Sane ametoa taarifa ya shukrani kwa timu yake ya taifa kwa kumruhusu kuondoka wakati wakijiandaa kupambana na Peru, wakati huo ametoa taarifa pia ya kupata mtoto wa kike jana usiku, ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter. anasema “Ninafurahi kuwataarifu kuzaliwa kwa mwanangu wa kike jana usiku, mtoto na mama wanaendelea vizuri”.


Issa
Safi sana kwa sane kupata mtoto
Povel tz
Habar njema