Kocha wa Sassuolo Roberto De Zerbi amekiri kuwa Juventus ndio wababe wa Italia na Ulaya huku akisisitiza kuwa hiyo haimaanishi kuwa tayari wamewashindwa.
Sassuolo wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Serie A baada ya kucheza gemu 3 na kushinda mbili huku wakitoa sare gemu moja. Juventus ndio wanaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 9, pointi mbili mbele ya Sassuolo baada ya kushinda gemu zote tatu.
Kocha wa Sassuolo anasema anafikiria namna wanavyoweza kumshinda Juventus, akikiambia chanzo cha habari cha Italia cha Corriere dello Sport, alisema “Juventus wana nguvu zaidi kwa upande wa Italia, pia wana nguvu zaidi Ulaya katika msimu huu”
Roberto anadai anaangalia namna ya kuwazuia wababe hao, anaamini wataweza japokuwa hajui ni namna gani. Hata hivyo, anajivunia kuwa nafasi ya pili nyuma ya Juve. Kwakuwa anaamini bado hawajashindwa, basi ataonyesha jitihada zote kuhakikisha wanawakalisha wababe hao.


Issa
Mmh juve pakubwa sana
isha
duuh juve wanamkwara sawa acha tuone
Povel
Juve noma sana
Nasra
Juventus kiboko
Furahav
Iko juu juve.