Baada ya ushindi dhidi ya Inter Millan katika Fainali ya Europa. Mchezaji nyota wa Sevilla – Ever Banega atangaza kuikacha miamba hiyo ya soka la La Liga na kutimkia Saudia Arabia katika klabu ya Al- Shabab.
Katika mchezo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute, Inter Millan walipata goli la kuongoza mapema dakika ya 5 kupitia mkwaju wa penati kabla Luuk De Jong hajasawazisha na kuongeza goli la pili.
Kufikia mapumziko ya kipindi cha kwanza, matokeo yalikua n 2-2 na kunako dakika ya 90, matokeo yalikua ni 3-2 baada ya Lukaku kushiriki kwenye goli la kujifunga kwa kushindwa kuzuia mpira wa adhabu uliopigwa kwa umakini na Ever Banega.
Ushindi kwa Sevilla umewapa rekodi ya kuwa timu pekee iliyocheza fainali 6 za Europa na kushinda zote.
Akizungumza na Movistar, Banega amesema ” Sina maneno ya kusema kwa namna ninavyojisikia. Wakati huohuo ninapaswa kusema, ninaondoka kwenye klabu ya maisha yangu lakini nimeridhika.

“Ninaondoka na ubingwa mwingine, shukrani kwa wachezaji wenzangu, ninaondoka nikijiamini. Ninataka kuwashukuru wachezaji wenzangu wote kwa kufanikisha mimi kushinda kombe.Pamoja na benchi la ufundi kwa kutufikisha hapa.
“Sasa ninapaswa kufurahia kupeleka kombe kwa mashabiki wa Sevilla, watu ambao hawakuweza kuwa hapa lakini tunahisi uwepo wao.”
Uhusiano wa soka la La Liga na Ever Banega akiwa Sevilla.
Banega ameitumikia Sevilla kwa misimu 5 ndani ya miaka 6. Amehusika katika makombe 3 ya Europa lakini Sevilla hawakumuongezea mkataba wa kusalia kwenye timu hiyo msimu ujao.
Sasa ni rasmi, Banega atajiunga na miamba ya soka la Saudi Arabia – Al Shabab.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


magdalena
maamuzi yake yapo sahihi uenda kaona huko ndo panamfaa zaidi
Sauda
Safari njema.
Shan
Kila la kheri kwake
Mwajumah
Aende tu mm wala simkubali uyu mtu sijaona umuhim wake alipokua sevilla#Meridianbettz
aisha
Banega kila la kheri labda alikoenda kaona kuna manufaa zaidi
Shan
Kila lakher banega uwendako.
Sadick
Anaondoka kwa heshima kubwa na kumbukumbu nzuri kwa utumishi uliotukuka. Kila la kheri huko Arabuni#meridianbettz
jullie
kila la kheri
Nasra
Kila la kheri uendako
Caroline
Anaondoka lakini ameiletea Sevilla heshima kubwa
Lydia Emmanuel Magoti
Mamuzi yake nisahii kwasababu anangalia masilai sehemu panapo mlizisha ndipo ataweka kambi yupo sahii
Rehema
Kila la kheri
Adelta
Banega aende tu labda ashaona ndoto zake zipo Saudi Arabia@meridianbettz
Khadija
kila kheri uendako#meridianbettz
Issa
Banega safi umeitendea haki sevilla
Ernest
Banega amejitengenezea heshima na rekodi kubwa sana ndani ya Sevilla
Dorophina
Banega ameacha jina Sevilla watamkumbuka kila lakheri huendapo
felister
vizuri Kama unaondoka ukiwa umeridhia
Sylvester
Ni jambo jema amefanya Vizuri akiwa na Sevilla anatafuta changamoto mpya na kwenda kucheza mpira mwepesi kidogo
Tatu
Maamuzi aliyeyachukua banega mazuri kila LA kheri huko aendako
Neema
Safariii njemaa
marry
all the best
Amiri Kayera
Anaend taft changamot mpya
Saupha mohamed
Kila LA kheri
Zeiyana
Banage nadhani wakati wake wa kusepa sevilla ushawadia.
Shan
Kila la kheri kwake
Hope mwaikuka
It’s your choice
Povel
Banega inatosha lfy la Sevilla Kama vle muda wake umefika kwenda kusaka pesa nchi za china na uarabuni vle
Gabriel
Banange anaondoka kwa furaha sana 👍
Devotha
Kila la kheri
Rose kapinga
Riziki popote!!!!
Shafii
Kila lakheri banega huko uwendako.
Salma ngende
Safari njema
David Pere
Anaondoka kwa heshima kubwa na kumbukumbu nzuri kwa utumishi uliotukuka. Kila la kheri huko Arabuni
Ester jackson
Kila la laheri katika timu nyingine mana umeweka heshima Seville watakukumbuka sana kwa ushitikiano uliotoa na kupata ushindi wa kombe
farida ahmadi
Kila la kheri banega
Samiah
Safi
Furahav
Wasalimie uko uendako.
Sabrina
Hongera take namtakia kila la kheri uko aendako
Latifa juma mohamed
Banega anaondoka Sevilla lakini atakumbukwa Sana ameweka heshima kubwa na kila la kheri huko aendako.
warda
Sio mbaya hata akiondoka kawaacha vizuri
Chiku
Yani amejitaid kuweka mambo sawa