Baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na Barca, Dembele aliweka ngumu kuondoka klabuni hapo Januari mwaka huu licha ya ofa kuwepo mezani. Anataka nini?
Raisi wa Barcelona, Joan Laporta bado haelewi ni nini hasa anachokifikiria mchezaji huyo pamoja na wakala wake. Kuna uwezekano mkubwa asitumike tena kule Camp Nou baada ya klabu hiyo kumsihi aondoke klabuni hapo mwezi uliopita. Barca walifanya kila walichoweza ili kumsaidia Dembele kuondoka lakini, mchezaji aliweka ngumu kuondoka.

Kinachomshangaza zaidi Laporta ni ofa zilizotolewa na vilabu vya Uingereza ambazo, Dembele alizikataa zote. Kukataa kwake kuondoka pamoja na kugoma kusaini mkataba mpya, kunamfanya Laporta aamini kuwa, Dembele na wakala wake wanajua wanachokitaka lakini, hawakiweki wazi.
Kilichobaki sasa hivi ni uongozi wa Barca kuwa na majibu ya kubashiri. Inasemekana, wanahisi Dembele ataenda Man United au Juventus baada ya msimu huu kutamatika. Hii ni kwasababu, vilabu hivi vimeshawahi kuonesha nia ya kutaka kumsajili Dembele lakini, safari hii havijajitokeza kabisa licha ya kujua wazi, Dembele yupo sokoni.

Pamoja na hilo, United na Juve wanamahusiano mazuri na ya ukaribu sana na wakala wa Dembele na hivyo, mpango wao ni kukaa mezani baada ya Dembele kuwa mchezaji huru. Barca wanafikiria hivi. Swali ni – Je, fikra zao zinaendana na Dembele au kila mtu afikirie atakavyoweza?
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


