Klabu ya soka ya Barcelona imeeleza kua ina mpango wa kuwabakiza wachezaji wawili raia wa kimataifa wa Ureno Joao Felix na Joao Cancelo ambao wapo klabuni hapo kwa mkopo.
Kupitia Mkurugenzi wa michezo klabuni hapo Deco ameeleza kua klabu ya Barcelona ina mpango wa kuwabakisha wachezaji hao klabuni hapo kwa muda mrefu pindi ambapo mikataba yao ya mikopo itakapomalizika.Joao Felix amejiunga kwa mkopo wa msimu mzima klabuni hapo akitokea Atletico Madrid, Huku Joao Cancelo yeye akitokea klabu ya Manchester City na wote wanahitajika kwa mipango ya muda mrefu klabuni hapo.
Deco ameeleza ni mapema lakini wanapanga kufanya mazungumzo na vilabu vya wachezaji hao kwajili ya kuwabakiza klabuni hapo, Kwani wanavutiwa na wachezaji hao na wangependa waendelee kuitumikia Barca.Barcelona wanapitia kipindi kigumu kiuchumi jambo ambalo linaonekana kuwakwamisha kupata wachezaji wa levo ya juu na kuishia kupata wachezaji kwa mkopo, Lakini uongozi wa klabu hiyo umeahidi watahakikisha wanawabakiza wachezaji hao wenye ubora wa hali ya juu klabuni hapo.